SIMULIZI YA MFALME NA MCHAMUNGU. Siku chache baadaye, Mfalme akamchagua Farasi wake aliye bora na mzuri kuliko wote, akiwa na jopo lake la walinzi na wapambe akaingia mtaani akitembea tembea kufurahia nchi yake. Katika pitapita yake wakojikuta wapo sokoni, mbele yao kundi kubwa la watu limuzunguka wakishangaa kitu. Mfalme akauliza "pale pana nini"? Akaambiwa kuna mtu toka kusikojulikana amekuja na farasi mzuri ajabu, ni farasi wa kushangaza ambaye utatamani kumtazama. "Yani bwana mfalme hata wewe na ufalme wako wote hujawahi na hutawahi kumiliki farasi kama huyo". Mfalme akafura kwa hasira, kwamba kwenye nchi yangu raia tu amiliki kitu kizuri kuliko mimi Mfalme!!? Akajisemea hii sasa ni dharau, lazima nilishughlikie vilivyo HAIWEZEKANI.