Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

REAL MADRID YAWASILIANA NA COUTINHO


Real Madrid wanaamini wataweza kuipiku Barcelona katika mbio za kumsajili Philippe Coutinho, kwa mujibu wa Mundo Deportivo .
Baada ya jitihada zao kugonga mwamba kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili majira ya joto, Barca sasa wanataka kurudi upya kwa ajili ya kiungo huyo dirisha la uhamisho litakapofunguliwa Januari. Lakini Madrid imeibuka kuwa timu nyingine ambayo anaweza kujiunga nayo nyota huyo.
 
MAN CITY YAMFUKUZIA CAN


Manchester City wapo tayari kuchuana na Juventus kumwajili kiungo wa Liverpool Emre Can, kwa mujibu wa Calcio Mercato .
Mkataba wa Can unafikia kikomo mwisho wa msimu huu, na kutakuwa hakuna ada itakayohitajika kumsajili Mjerumani huyo.
 
JORDIN SPARKS na BRANDY.


Jordin+Sparks+Brandy+2016+Pre+GRAMMY+Gala+x3Tn5rAgxQ-l.jpg
 
REAL BADO WANA TUMAINI LA KUMPATA NEYMAR


Real Madrid wanapanda mbegu kumsajli Neymar siku za mbeleni licha ya Mbrazili huyo kuhamia PSG kwa uhamisho wa rekodi ya dunia miezi michache iliyopita, kwa mujibu wa Diario Gol .
Ripoti zinadai kuwa Mbrazili huyo anataka kutwaa Ballon d'Or na Ligi ya Mabingwa akiwa Paris ndani ya miaka miwili. Ikiwa hatafanikiwa kutimiza malengo haya, basi Neymar atatafuta njia ya kutokea.
Inaaminika rais wa Real amekuwa kwenye mawasiliano ya karibu na baba wa mchezaji huyo ambaye pia ni wakala wake, na amesisitiza kuwa milango ya Real Madrid itakuwa wazi kwa daima.
 
CONTE AMEBAKIWA NA KIPIGO KIMOJA KUFUKUZWA CHELSEA


Meneja wa Chelsea Antonio Conte anaweza kufukuzwa kazi ikiwa atafungwa na Manchester United Jumapili kufuatia tofauti baina yake na mmiliki Roman Abramovich, kwa mujibu wa habari mchanganyiko.
The Times limedai kuwa kipigo dhidi ya mahasimu wao wa Ligi Kuu Uingereza - ambacho kitawafanya wawe na pengo la pointi 12 dhidi ya vinara wa ligi - kitamweka Conte katika wakati mgumu.
Conte na kikosi cha Chelsea, ambao walikuwa mabingwa wa ligi msimu uliopita, waliangaliwa katika mazoezi wiki hii na bilionea huyo.
 
MESSI AMKATAZA AGUERO KUJIUNGA NA REAL MADRID


Lionel Messi amemshauri Mwargentina mwenzake Sergio Aguero kutojiunga na Real Madrid mwaka ujao, kwa mujibu wa Diario Gol .
Rais wa Madrid Florentino Perez amemtaja straika wa Manchester City, Aguero kuwa mchezaji sahihi na anaamini ataweza kumshawishi kujiunga na Blancos ikiwa Pep atamsajili Alexis Sanchez.
Lakini kwa mujibu wa habari Lionel Messi amemtumia ujumbe Aguero kwa njia ya WhatsApp, na amemwambia rafiki yake kipenzi na Mwargentina mwenzake kuwa ni vema abaki Manchester kwa sababu Madrid inaelekea kuporomoka na City wanazidi kuwa tishio chini ya Guardiola kwa sasa.
 
BETIS YAANDAA DAU KUMSAJILI WILSHERE


Real Betis wanajipanga kufanya jaribio jingine kumsajili Jack Wilshere, kwa mujibu wa The Sun .
Kiungo huyo wa Argentina alikataa kujiunga na klabu hiyo ya Hispania msimu uliopita ili aendelee kubaki London Kaskazini. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amerejea kibaruani baada ya kupona majeraha yake, lakini bado hajapata nafasi kikosi cha kwanza.
 
SPURS YACHUANA NA ARSENAL KUMSAJILI GORETZKA


Tottenham Hotspur wanataka kuungana na Arsenal kuiwania saini ya to sign Leon Goretzka kutoka Schalke, The Mirror limeripoti.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa kwenye rada za Gunners kwa muda mrefu na anaendelea kuzivutia timu nyingi barani Ulaya. Inaaminika kuwa Spurs wamefuatilia mechi zote alizocheza na awanaweza kufanya jitihada za kumsajili kwani mkataba wake unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
 
MAN UTD WANAMTAKA DONNARUMMA KUMRITHI DE GEA


Jose Mourinho amekuwa akiwasiliana na Gianluigi Donnarumma akimtaka kipa huyo wa AC Milan kuchukua nafasi ya David de Gea Manchester United, kwa mujibu wa Don Balon .
Imeripotiwa kuwa De Gea anataka kuondoka Old Trafford msimu ujao wa majira ya joto baada ya kuitumikia United miaka saba, na PSG wanapewa nafasi kubwa kumsajili Muhispania huyo aliyeko kwenye rada za Real Madrid.
 
Back
Top Bottom