Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5. Unachotakiwa kujiuliza, je, ukipewa nafasi ya kuishi miaka 90, utakuwa na pesa za kukuwezesha kuishi miaka hiyo au utategemea msaada kwa watoto wako na watu wengine, tafakari hilo kama utaona hutajiweza, kisha weka utani pembeni na ongeza juhudi sana za kutafuta pesa.
 
7. Haina haja ya kulalamika sana, unatakiwa ujifunze kwa bidii na hadi ukaelewa namna ya kuongeza pesa ulizonazo zikawa hata mara tano. Huhitaji wewe mshahara mkubwa. unachohitaji ni juu ya kujua jinsi unavyoweza kuongeza pesa ulizonazo na ukafanikiwa kwa asilimia kubwa.
 
8. Ikiwa leo maisha yako ya uzeeni yataishia kwenye umaskini, sio swala la kumlaumu Mungu. Unatakiwa kujilaumu wewe kwa kushindwa kwako kufanya uchaguzi sahihi wa kupanda katika kipindi cha kupanda na kuvuna katika kipindi cha mavuno na si kuwa ombaomba.
 
8. Ikiwa leo maisha yako ya uzeeni yataishia kwenye umaskini, sio swala la kumlaumu Mungu. Unatakiwa kujilaumu wewe kwa kushindwa kwako kufanya uchaguzi sahihi wa kupanda katika kipindi cha kupanda na kuvuna katika kipindi cha mavuno na si kuwa ombaomba.
 
9. Mkakati wa kuwekeza kwa muda mrefu unatakiwa uwe na mambo haya yafuatayo:-
Moja, wekeza kila mwezi, kwa muda usiopungua miaka 20 kutokana na kipato unachokipata bila kujali kipato hicho ni kidogo kiasi gani.
Mbili, wekeza kila mwezi bila kujali, huo mwezi ni una Tsunami, una maafa au mwezi una mafuriko ya kiasi gani. Ila unachotakiwa kufanya ni kuwekeza angalau kila mwezi kwa kile unachokipata, hakuna haja ya kutoa sababu au kisingizio chochote.
 
10. Ukitaka kujenga utajiri wako na ukafika mbali kweli, amua kuujenga utajiri wako kama kobe. Chukulia kama hizo ni mbio za muda mrefu, usikurupuke kujenga utajiri wako utakwama sana.
Fanyia kazi misingi hii na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
 
Mbinu Za Kujitengenezea Maisha Mengine Nje Ya Ajira.

Inawezekana ukawa umeajiriwa na miaka nenda na miaka rudi hujawahi kufanya kitu cha msingi, au inawezekana bado umeajiriwa na unasubiri mafao tu. Ninachotaka kukwambia ni kwamba ni lazima uwe na akili nyingine ya ziada itakayokufanya uweze kutengeneza maisha mengine zaidi ya ajira uliyonayo.
 
Na hayo maisha mengine ili uweze kuyaishi hayo unaweza kujikita katika kufanya biashara au kujiingiza katika suala zima la kufanya ujasiliamali. Haiwezekani ukaendelea kuishi kwenye ajira tu peke yake miaka nenda rudi, kipo kipindi uwe na uhakika utakwama kama usipoingia kwenye ujasiriamali.
Na ili uweze kufanya hivyo unatakiwa kufanya mambo yafutayo;-
 
1. Dhibiti matumizi yako ya pesa.
Moja kati ya matatizo ambayo yanayowakumba watu waliojariwa ni kwamba wanashindwa kudhibiti matumizi yao ya fedha, Wengi wao wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu wana imani hata pesa ikisha mwisho wa mwezi wana uhakika wakupa pesa nyingine.
 
Kwa minajili hiyo ndio maana watu hao wanashindwa kuanzisha miradi ya msingi na hivyo kupelekea watu wao kuwa na matumizi mengi ya pesa. Hivyo ili uweze kuanzisha mradi wako ukiwa umejiliwa hakikisha unadhibiti kiwango chako cha matumizi ya pesa katika kila mshahara unaopata.
 
2. Usitegemee kipato kimoja.
Jambo la pili ni kwamba ukiwa bado umeajiliwa hakikisha ya kwamba hutegemei kipato kimoja cha kukupatia pesa, bali kuwa na vyanzo vingi vya kuweza kujingizia kipato wewe mwenyewe. Ili kufanya hivyo ni vyema ukajikita katika masuala ya ubunifu na ujasiliamali kwa ujumla.
Kubaki na kipato kimoja ni hali ya hatari sana kwako. Unatakiwa una vipato vingi ambavyo vitakuwezesha wewe kuweza kuishi maisha nje ya ajira. Ikiwa hautafanya hivyo itabaki kwako hadithi ya kutokufanikiwa. Ni muhimu sana kutengeneza vyanzo vingi vya pesa ili kuishi maisha nje ya ajira.
 
3. Tumia mshahara kuanzisha mradi.
Katika hili ni kwamba ili uweze kujitengezee maisha mengine nje ya ajira, kwa hicho kiwango kidogo au kikubwa cha mshahara unachokipata hakikisha ya kwamba unatenga asilimia fulani kwa jinsi utavyoona wewe ili kuanzisha mradi wako binfsi itakayokufanya ufurahie maisha unayoishi.
 
Mweeee hajipendi eee au kasahau mwanzoniiiiiii kuleee hahaha
Nilipitia majuzi kule nilicheka saaaaana,mara akaenda Masaki,akafurumushwa na... Ile kurudi njiani nakutana na carba ameumizwa na Kichwa kichafu baada ya kuvalishwa pete ya visoda watu watatu.
Maisha haya jamaniii[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom