Msanii wa filamu na mjasiriamali Jackline Wolper amefunguka na kumkumbusha Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kuchukua hatua kwa watu ambao wamekuwa wakionyesha makalio yao kwenye mitandao ya jamii. Wolper amesema hayo leo hii baada ya kuona watu bado wanaendelea kuweka video na picha zikionyesha makalio yao wakiwa nusu uchi na kusema kuwa hilo jambo linamshangaza mpaka jasho la damu linamtoka. "Haki ya ukweli yule kiongozi wakukomesha vichupi yuko wapi, mbona bado tunaona makalio Insta au ndio sanaa kila sehemu mimi nashangaaa mpaka jasho la damu linanitoka chaaaaa" alisema Wolper