Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mimi??? Ndoa ya yego[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hivi kwenye harakati zake huku akisindikizwa na vimaua vya kichoyo na viglasi nusu mvinyo mwekundu amewahi kufanikiwa hata siku moja?

Data given:
1.Pimbi=failure(carba's formula)
2.Kichwa kichwa= Pimbi
3.Cole Williams=Kichwa kichafu
4.Yegomasika=Cole Williams

Since 4=3,3=2,2=1...
Therefore 4=1(by similarities formula)

[emoji124] [emoji124] [emoji124] Pole sana andaetini wetu[emoji120] [emoji120]
Dah hatari sana[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
LOL! Inasikitisha Mkuu kuona nchi yetu ambayo kwa maoni yangu kutokana na utajiri mkubwa wa rasilimali ilitakiwa iwe inafanya vizuri sana kwenye kila sekta sasa imekuwa ni kichwa cha mwendawazimu. Kuna wakati huwa nataka kubwanga manyanga lakini nikikumbuka maneno ya Baba wa Taifa nasema acha tu nipambane. Na huu waraka wa Maaskofu umenipa nguvu mpya kumbe watu kama BAK hatupo pekee yetu maana tunaambiwa siye ni wapiga maadili, tuna bifu na jamaa wakati ukweli hauko hivyo. Huyu akifanya mazuri kwa faida ya Watanzania wote bila ubaguzi mie nitakuwa wa kwanza kusimama na kupiga makofi.

Bunge likiachwa lifanye kazi yake kama Bunge kwa faida ya Watanzania mie nitapongeza, mahakama zikiwa huru kwenye maamuzi yake mie nitapongeza. Mshikamano miongoni mwetu ukipaliliwa badala ya kuvunjwa vunjwa kwa faida yetu na vizazi vyetu vijavyo mie nitapongeza. Watanzania wakipewa uhuru wa kuikosoa Serikali na viongozi wake na pia vyama vya upinzani kuachiwa kufanya yao kama katiba inavyoruhusu mie nitapongeza lakini mhhhh! Ngoja niishie hapa Mkuu kule siasani nimepumzika saa hizi.
Well said bro Nina mengi ya kusema wacha nisubiri muda utaongea
 
Sawa na pole mkuu...

Kuna makala naziandika pengine nitakupa uzisome kwanza kabla sijazipeleka ninakotaka kuzipeleka, halafu unipe maoni yako. Viongozi wa Afrika wana matatizo yanayofanana fanana. Najaribu kudodosa tatizo lilipo na masuluhisho yake...kwa mtazamo wa kisaikolojia...
Tungepa masuluhisho ingekuwa poa sana naangalia ukanda wetu huu Uganda na M7 ,Rwanda na kagame ,Burundi na Nkurunziza ,Congo DRC na Kabila, Angola na Dos Santos ,ni shida sana Bila sahau Sudan na Barre yaani sometimes maneno ya Trumb yanaishi
 
Sijaelewa hii shimba ufafanuzi please
Nadhani ni kejeli kwa dhana nzima ya uumbaji. Kule Uswizi milimani kuna limtambo likubwa lenye hilo jina na wanasayansi wako huko wanagonganisha particles mbalimbali zikiwa katika mwendo karibu na spidi ya mwanga ili kuiga (mimic) hali iliyokuwepo pale mwanzoni kabisa mwa Big Bang. Mwaka juzi nadhani walitangaza kugundua particle moja iitwayo Boson, particle ambayo imepachikwa jina la particle ya Mungu. Inasemekana kuwa particle hii ndiyo inashikilia universe nzima na ndiyo ina uzito mkubwa unaokamilisha universe na kuifanya iwe hivyo ilivyo. Uwepo wa particle hii ulitabiriwa kinadharia katika mahesabu ya mwanasayansi mwenye jina hilo na baadaye ikagusiwa pia na akina Einstein na juzi juzi hapa na Stephen Hawking alipokuwa anaunda nadharia yake kuelezea black holes (ambazo nazo zilitabiriwa katika mahesabu ya Einstein alipounda nadharia yake ya General Relativity).

Hapa nadhani ni wanasayansi wanawasha hilo limashine ili kuumba universe. Dhihaka. Kejeli. Mzaha. Ulimwengu uliumbwa kwa kanuni zinazoeleweka tu na ambazo wanasayansi wanajitahidi kuzielewa na kuzifafanua kila leo - kinadharia na kimajaribio !!!
 
Back
Top Bottom