Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mafuta yatokanayo na mimea huwa katika hali ya kumiminika kwenye joto la kawaida, mara nyingi mafuta haya hayana lehemu, ni vizuri kutumia mafuta haya kwani ni bora kwa afya ya mlaji ukilinganisha na yale ya viwandani.

Nimekuwekea orodha ya Mafuta yatokanayo na mimea pamoja na mbegu zitoazo mafuta kama ifuatavyo:

Mafuta ya Soya
Mafuta ya Ufuta
Mafuta ya Alizeti
Mafuta ya Karanga
Mafuta ya Pamba
Korosho
Kwembe
Maboga
 
FAIDA ZAKE :

Hupunguza Lehemu mbaya kutokana na kutokuwa na lehemu.
Mafuta haya yana Omega3 ambayo ni muhimu kwa kuondoa Lehemu mbaya mwilini na kulinda mwili usipate na magonjwa ya moyo.
Mafuta haya yana 3 Pufa (n-3 Pufa)(Poly unsaturated fat) haya ni aina ya mafuta yanayotokana na Mchele, Soya, Ufuta na Pamba.
Huleta afya nzuri na kulinda mwili usipate na magonjwa kama vile Kisukari, Kansa, Magonjwa ya moyo, Upungufu wa nguvu za kiume na kike.
Mafuta haya ni rahisi kuyeyuka na kuleta ladha nzuri katika chakula.
Vyakula vilivyo na mafuta yenye asili ya mimea ni pamoja na Mafuta ya Karanga, Alizeti, mafuta ya Zaitun(Oliver Oil), Pamba, Korosho, Pistachio, Dona, Maharage ya Soya na mchele wa kutwanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…