Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatuna presha na mechi hiyo na wala hatudharau bali tunaingia na sura ya kupambana na heshima ya klabu yetu, mashabiki watakuwa nyuma yetu tunakwenda vitani tukiwa kamili.
 
MATTEO AGEUKA KIPA

Mshtuko mkubwa kwa Yanga ni majeruhi wa ghafla kuibuka katika kikosi chao hasa eneo muhimu la makipa na kilichokuwa kikiendelea kama angeumia kipa kinda Ramadhan Kabwili basi mashabiki walitakiwa kujindaa kisaikolojia kwa straika wao Matheo Anthony ndiye aliyeandaliwa kuwa kipa, lakini kocha wao Zahera akasema tulieni Youthe Rostand yuko sawa.
 
Jana asubuhi Rostand alikuwa hajisikii vizuri na kuleta wasiwasi, lakini wakati raia huyo wa Camaroon akishtua hivyo tayari kipa namba mbili wake Benno Kakolanya hakuwepo kabisa baada ya kushtua maumivu ya mkono wake.
 
Udhuru huo wa makipa hao wawili ukaifanya Yanga kusalia na kipa mmoja tu Kabwili na asubuhi akachukua lango moja huku la pili sasa ndiye aliyeibua mjadala na Matheo akachukua ‘glovu’ akasema nakaa mimi hapa twenda kazi.
 
Mazoezini hapo likapigwa soka la ukweli na Matheo hakutania kumbe jamaa anajua na jaribio lake kubwa lilikuwa ni lile la Mhilu aliyepenyezewa pasi ya maana na Tshishimbi kisha kinda huyo kupiga krosi safi ikamkuta kiungo fundi anayejua kufunga Raphael Daudi akaachia shuti kali ebwana Matheo akalicheza kama Gigi Buffoni wa Juventus.
 
Amen
 
Hata hivyo, wasiwasi wa makipa hao uliondolewa baada ya kubainika kumbe Rostand alikuwa amepewa mapumziko maalumu ili awe sawa na leo ataanza mwenyewe golini akisaidiwa na Kabwili, ambaye alirejea haraka katika kikosi hicho akitokea DR Congo walipoenda kuichapa timu ya vijana ya huko.
 
TEGETE AWAJAZA UPEPO

Kocha mkongwe na anayetajwa kuwa mnazi wa kutupwa wa Yanga, John Tegete amewataka Yanga kutulia na kupunguza presha uwanjani watakapowakabili Simba leo Jumapili pale Taifa.
 
Nasubiria hio baadae[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…