Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi itakuwa kati ya timu ambazo zimefunga mabao mengi zaidi msimu huu huku washambuliaji bora zaidi duniani wakikutana.
Real Madrid wanatafuta ushindi wa 13 na wa tatu mfulizo huku Liverpool wakiweza kupanda juu ya Bayern Munich na Barcelona nyuma na AC Milan katika orodha ya vilabu vilivyopata ushindi mara nyingi zaidi katika European Cup na Champions League ikiwa wataibuka washindi huko Kiev.
 
Milner anaweza kuwa na umuhimu usiotarajiwa Kiev?
Zikiwa zimefunga zaidi ya mabao 90 kwenye mashindano yote msimu huu ni wazi kuwa fainali hii itakuwa kama vita kati ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Mohamed Salah wa Liverpool.
Wote wako mbioni kun'gang'ania tuzo ya Ballon d'Or mwishoni mwaka 2018, lakini pia kuna mwanamume ambaye bila kutarajiwa huenda akawa mwenye umuhimu mkubwa huko Kiev.
James Milner alionyesha ubabe wakati wa nusu fainali dhidi ya Roma wakati alifikisha mchango wake muhimu katika mechi hadi mara 8 msimu huu na kusawazisha rekodi iliyowekwa na Neymar mwaka 2016-17.
 
Ni nani anakumbwa na harakati zaidi katika safu ya ulinzi?
Wakati wa kuanza kwa msimu kulikuwa na shaka kuhusu safu ya ulinzi ya Liverpool, lakini kufuatia kuwasili kwa Virgil van Dijk mwezi Januari na kuimarika kwa kipa Loris Karius inamaanisha kuwa tena hakuna udhaifu.
Kwa Real ni kitu tofauti.
 
Walikosa mchango wake Sergio Ramos wakati wa duru ya pili ya mechi kati yao na Juventus.
Liverpool nao wana matatizo yao, wameshindwa mara 13 kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ikiwemo mara sita dhidi ya Roma na sare yao ya mwisho.
Lakini kikosi hicho cha Jurgen Klopp kimeshinda mara sita mfululizo msimu huu rekodi iliyowekwa na Barcelona.
 
Mashabiki wa Liverpool wameendelea kusafiri umbali mrefu kutoka Uingereza kwenda Kiev. Kwa ajili ya fainali ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Real Madrid, mfano mmoja alikuwa anasema ametumia siku nne akipitia Sweden, kisha anaingia Latvia, anaingia Lithuania kisha Ukraine
Mshabiki mwingine amesema anatokea mjini Liverpool akipanda Train mpaka Glasgow, pale Glasgow anapanda Ndege mpaka Palanga nchini Lithuania kisha anakodi gari kama saa tatu njiani hivi kueleka uwanja wa ndege wa Vilnius hapo anapaa kuelekea Kiev.
 
Steven Thompson, 33, yeye anafunga ndoa leo, amekata tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi ambapo mpango ni arejee Jumapili ili aende kwenye fungate na ambaye sasa atakuwa mkewe Bi Rachael.
Rachel amekubali mumewe aende akatimize mapenzi yake kwa mpira wa miguu lakini arejee jumapili waende fungate Australia. Sasa Steven anasema sawa huyu ameniruhusu na huenda amekasirika kiasi, ila hofu yangu ni ikiwa nitaikosa ndege ya jumapili.
Fainali ya klabu bingwa ulaya inapigwa hapo kesho, Nani ataibuka na kicheko? Christiano Ronaldo na Real Madrid yake au Mohamed Salah na Liverpool?
 
Ronaldo: Mimi na Salah ni tofauti kabisa mimi mrefu yeye kidogo mfupi anacheza na mguu wa kushoto nacheza na wakulia na nacheza mipira ya vichwa watu wasinilinganishe na mchezaji yoyote nachowezasema amekuwa na wakati mzuri sana msimu huu tusubiri tuone
Maneno ya wivu hayo, kutamba kote alikotamba bado anasumbuka na mafanikio ya wengine!!!? Maneno ya aina hiyo awaachie mashabiki, vinginevyo tutamuona ni mwenye roho mbaya
 
Back
Top Bottom