Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatimaye mchezo uliosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, wa fainali za Kombe la Dunia 2018 unatarajiwa kupigwa kesho kati ya Ufaransa na Croatia.
Katika mchezo huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Luzhniki, Moscow, sio tu utampata bingwa wa Dunia, lakini ndio unaotarajiwa pia kumtangaza mchezaji atakayetwaa tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Dunia.
 
Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo ni nahodha wa Croatia, Luka Modric na kiungo mkabaji wa Ufaransa, N’golo Kante.
Tuzo hiyo mwaka 2002 ilitwaliwa na mshambuliaji mahiri wa Brazil, Ronaldo Nazario de Lima, 2006 ikatwaliwa na nahodha wa Ufaransa, Zinedine Zidane, 2010 ikatwaliwa na mshambuliaji wa Uruguay, Diego Forlan na 2014 Lionel Messi, akaitwaa tuzo hiyo.
 
Ingawa kwa kanuni za Fifa sio lazima mchezaji bora wa mwaka atokane na timu iliyotwaa ubingwa wa Dunia, lakini Luka Modric na N’Golo Kante, wanapewa nafasi kubwa kutokana na mchango wao binafsi ulioziwezesha timu zao kufika fainali.
 
Wote wawili wameziwezesha timu zao kufika fainali, Modric akiingiza Croatia fainali ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, Kante naye anaonekana kukaribia kuipa Ufaransa taji la pili la ubingwa wa Dunia.
Mbali ya Modric na N’Golo Kante, pia mshambuliaji kinda wa Ufaransa, Kylian Mbappe na kiungo Paul Pogba, wanayo nafasi ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na kung’ara kwao.
Pia Antoine Griezmann wa Ufaransa, Ivan Perisic, Mario Mandzukic na Ivan Rakitic wa Croatia, wanayo nafasi ya kutwaa tuzo hiyo.
 
Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Italia, Jorginho kutoka Napoli baada ya Manchester City kujiondoa katika mbio hizo kutokana na dau la pauni 50milioni.

Jorginho (26), amesaini mkataba wa miaka mitano na kujiunga na bosi wake wa zamani wa Napoli, Maurizio Sarri aliyetua Stamford Bridge.
 
Alhamisi, City walihakikishiwa na wakala wa Jorginho kuwa kiungo huyo atajiunga nao, lakini rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis alisema mchezaji huyo atajiunga na Chelsea.

"Nimefurahi sana kupata nafasi ya kujiunga na Chelsea," alisema Jorginho.
 
Sijambo rahisi kuwa sehemu ya timu kubwa kama hii, nimefurahi sana. Natamani kuanza kucheza katika ligi yenye ushindani nikiwa na timu yenye lengo la kushinda kila taji."

Jorginho alijiunga na Napoli mwaka 2014, msimu uliopita alifunga mabao manne katika michezo 36 na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Serie A.
 
Pia, alifunga penalti katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambao Napoli ilifungwa 4-2 na Manchester City Novemba mwaka jana pia alichezea Italia ilipolazimishwa sare 1-1 na England mwezi Machi.
 
Hahahahaha [emoji16] [emoji16] [emoji16] hakuna gharama yoyote. nawaamini sana blues, inadaiwa Deschamp ameonekana mjini Kanu Nigeria ameenda kutafuta mbinu za ziadi za ushindi[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
Croatia wakiwa na Rais wao Mrembo kolinda Wanacheza kama tembo aliyejeruhiwa wako vizuri sana hii WC yao kabisa
 
Back
Top Bottom