Mara alama za vidole. Mara hivi. Sijui pasipoti za kielektroniki. Vitambulisho vya taifa. Kuna ajenda kubwa hapa. Kuwabana watu. Kuwafuatilia vizuri. Big Brother yupo kila mahali. Na hizi ni dalili za mwanzo za udikteta. Na ukiinua kichwa tu unagongwa. Wana alama za vidole. Na sura ya kila mtu. Ndiyo silaha kubwa ya Wachina hii. Watu mabilioni wote wametulizwa...Kimyaaaa !!!
Obama alipitisha sheria nyingi sana zilizoingilia maisha ya Wamarekani moja kwa moja. Mpaka vyakula wanavyopaswa kula watoto mashuleni. Bima za afya kwa lazima...Amekuja "kichaa" Trump amezifuta zote. Hoja yake kubwa ni kwamba serikali isiingilie sana maisha ya watu. Mtu ale anachotaka. Hata akiamua kutokuwa na bima akiugua afe ni halali yake. Ndiyo maana ya uhuru...Serikali kazi yake kulinda raia. Na kutoa huduma za umma...kwa mfumo uliopangwa. Mengine haya watu wawe huru...
View attachment 1329726