Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Niliwahi kupata homa kali ya mafua na kifua kikavu kikali, feb 2019, nakumbuka hata niliambukiza watu wawili hapa nyumbani na mmoja alizidiwa sana, lakini wote tuli survive.
Sijajua kama hiyo ilikuwa ndiyo yenyewe
 
Kama upo hapo kijijini si utapika mwenyewe vile unavyotaka, kwani watakulazimisha ule samaki wasio na viungo.
Vinginevyo mto Songwe na mito mingine kuna samaki wa kila aina pamoja na wenye magamba.
Ukifika kwenu usijipe unyonge, jitahidi kujichanganya, maana kila mtu ana kwao
Kwa kweli mimi mapishi ya vijijini yameshanishinda, samaki gani wasiowekwa viungo.

Kwanza kabisa mie samaki wa maji baridi na wasio na magamba huwa sili, mixer akose viungo sasa uwii ndiyo naweza hata nikatapika na walivyo na shombo vile.
 
Jifunze kuogelea bhana, usiniangushe.
Ila maji ya vijijini nayaogopa kuna mamba
 
Pande za kwenu ndo huwa tunaambiwa kuna nyoka wengi wenye sumu na hivyo kuna mabingwa wengi wanaotibia madhara kugongwa na nyoka.
Namshukuru Mungu sijawahi ng'atwa na nyoka ingawa nimepoteza baba wadogo wawili waliofariki baada kung'atwa na nyoka.
Inasaidia pia ukijua kama ana sumu ama la...Nilishawahi kuumwa na joka wakati tunavuna mahindi nikalikanyaga. Madawa ya wazee wa kijijini yakanisaidia hata hospitalini sikupelekwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…