Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. TRUMP ALIWAHI KUKATAA WATU WEUSI KUHESABU PESA ZAKE!Trump alikataza kampuni zake kuajiri wahasibu weusi kwa sababu alikuwa hataki hela zake zihesabiwe na mtu mweusi! Tuhuma hizo zilitolewa na John O’Connell ambaye alikuwa mwajiriwa wa moa ya kampuni za Trump.Katika moja ya vitabu vyake, Trump aliwahi kuandika kuwa maneno ya John O’Connell huenda kuwa yalikuwa na ukweli.
 
5. KAMPUNI YAKE YA KUPANGISHA NYUMBA ILIWAHI KUSHTAKIWA KWA UBAGUZI WA RANGI

Trump amekuwa akisikika kwa maneno yake ya kibaguzi kwa watu weusi. Hiyo siyo kwenye siasa tu, kuna wakati kampuni yake ya nyumba za kupanga ilishtakiwa kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi na ilithibitishwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mahakamani kuwa waliambiwa na wakubwa wao kuwapa watu weusi maneno ya kukatisha tamaa kuhusu nyumba zinazopangishwa.
 
10. ALISABABISHA WAKE ZAKE WA ZAMANI IVANA ZELNICKOVA WINKLMAYR NA MARLA MAPLES WAPIGANE.

Akiwa bado kwenye ndoa na Ivana, Trump alianza kuchepuka na Marla, baada ya Ivana kugundua hilo alimuanzishia timbwili Marla walipokutana naye kwenye mgahawa.
 
12. NI SHABIKI MKUBWA WA MIELEKA

.Amekuwa akiandaa mapambano mengi sana katika hoteli zake, huku pia akiwa mhudhuriaji mzuri wa mapambano hayo. Mwaka 2007, Trump na bilionea mwenzake, Vince McMahon, walibeti katika pambano fulani. Trump alishinda na akamnyoa nywele McMahon mbele ya kadamnasi.
 
Daah maalim seif alipoteza muda sana bora angekua anaandaa kakijana ka kuja kutikisa tena chaguzi za mbelen
Zanzibar hakuna tena mwanasiasa kijana mwenye ushawishi wa kuongea, kuwa na msimamo, kuridhika kimaisha na anayeweza kuwaliwaza wananchi kama maalim seif……..
wanamuandaa shemegi yake amani karume, muheshimiwa mansuri yussuf himid
 
14. ALIGOMBEA URAIS MWAKA 2000

Kwa mara ya kwanza Trump alijaribu bahati yake mwaka 2000 kwa kutafuta nafasi ya kugombea uraisi kupitia chama cha Democratic. Licha ya kukosa nafasi hiyo, Trump alishinda katika majimbo ya Michigan na California.
 
16. BUNGE LA UINGEREZA LILIPIGA KURA KUAMUA KAMA TRUMP ARUHUSIWE AU ASIRUHUSIWE KUINGIA NCHINI HUMO.Waingereza zaidi ya 250000 waliasaini waraka wa kumzuia Trump kuingia nchini mwao, hali hiyo ilililazimu bunge la nchi hiyo kujadili jambo hilo. Hata hivyo bunge lilimruhusu Trump kuingia Uingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…