Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukiamka unakimbilia kufanya nini? Utafiti umeonesha ya kwamba wengi tumeathirika na jambo moja kukimbilia simu na kuanza kuangalia watsapp, face book, twitter, Instagram. Tunahitaji kubadili kwani si tabia njema. Saa moja ya kwanza baada ya kuamka kitandani ni ya muhimu sana kujua unaanza na kitu gani cha kwanza ila isiwe simu.
 
Hakuna kanuni ya kipi uanze nacho lakini kutokana na umuhimu wa saa moja ya kwanza kuwa na umuhimu sana juu ya mstakabali wa siku yako nzima basi ni vyema kuanza na chochote kati ya hivi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuianza siku ila kamwe usianze na kushika simu. Mambo machache unayotakiwa kuhakikisha unayafanya katika saa yako ya kwanza ni pamoja na:-
 
Anza kwa kumshukuru Mungu kwa kuiona siku nyingine nzuri na jisemeshe ya kuwa unakwenda kuiishi siku kana kwamba ndio siku yako ya mwisho kuishi hapa duniani na unataka kuacha historia ya kuwa siku ya mwisho ulifanya makubwa sana na kama ungepewa siku zingine ungeushangaza ulimwengu.
 
Jiambie ya kuwa siku ya leo utajituma sana kuhakikisha hakuna ulichopanga kitakacho bakia paipo kukifanyia kazi. Endelea kujisemesha ya kuwa wewe u bora sana na utafanya kila jambo kwa ufanisi wa hali ya juu. Fanya hivyo kila siku. Futa kwenye ubongo wako msamiati wa kuahirisha.
 
Anza na kutahajudi. Kama kuna moja ya jambo nyeti katika maisha ya mwanadamu basi ni kutahajudi maana hapa unampa nafasi Mungu aongee na wewe. Kama utaweza kutumia saa nzima kutahajudi utaharakisha sana safari yako ya mafanikio. Maana mara baada ya kutahajudi utapata mawazo mbali mbali na hakikisha unayanakili yote kwenye kijinoti buku chako (Brain Damping note Book)
 
Anza kwa kujisomea kitabu chenye kukupa hamasa na kukufundisha mambo yatakayokusaidia kuboresha maisha yako. Sijui u mahiri katika eneo lipi – kikubwa hakikisha unaendelea kujiongezea maarifa katika hilo eneo lako kila siku. Kikubwa katika saa yako moja baada ya kuamka usiruhusu kuangalia TV na wala usichezecheze na watoto wala paka wala mbwa. Hakikisha umejitenga wewe peke yako katika utulivu wa hali ya juu. Ukiwa unajisomea hakikisha una mahali pa kuandika mambo ujifunzayo kwenye hicho kitabu.
 
Hakikisha kila siku kabla ujaianza siku lazima utokwe na jasho. Hili ni tendo muhimu sana. Tokwa jasho kabla hujaanza siku. Vitu vitakavyo kusaidia kutokwa jasho ni pamoja na kurukaruka Kamba, kukimbia angalau km 2 hakikisha hazipungui. Hichi ni kiwango mahususi. Hivyo kimbia au tembea km 1 kwenda na kurudi km 1. Endesha baiskeli. Tendo hili hata upangeje siku yako ni lalazima kulifanya. Hii itakuhakikishia kuianza yako ukiwa na nguvu za kutosha kufanya maajabu
 
Kunywa maji ya kawaida ila ni vizuri sana kama utaweza ya vuguvugu – kiwango cha maji ya kunywa kitategemea na uzito wako. Kanuni ni kuchukua uzito wako kwa kgs na kisha gawa kwa 24 jibu ni kiwango cha lita za maji ambazo ni lazima uzinywe asubuhi kabla ya kuswaki. Kwa nini unasisitizwa kufanya hivyo:-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…