antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 51,723
- 134,757
TrueWema unaigizika,utu hauigizwi. Si kila mtenda wema hadharani anafanya hivyo sababu ana utu.Mtu anaweza kuonyesha wema kwa wale ambao ana maslahi nao na kuwapenda lakini akawa katili dhidi ya wale asio na maslahi nao.Ndio kusema,utu ni mbeleko ya wema,ila wema si mbeleko ya utu."
👍Furaha na raha si lazima viende pamoja. Unaweza kuwa na kimoja ukakosa kingine. Na wakati mwingine unalazimika kukosa kimoja ili upate kingine. Wenye furaha wana amani, si lazima wawe na raha
🌹Kuweka akiba ya maneno ni pamoja na kukwepa kutumia maneno yenye kuhitimisha kama 'kamwe', 'asilani', 'daima', 'kila mtu' au 'wote'. Penda kutumia 'labda', 'pengine', 'huenda', 'kwa kiasi kikubwa' haya yatakupa fursa ya kujinasua mbeleni"
👍Iko miti ya kivuli, iko miti ya dawa, iko miti ya mbao, iko miti ya matunda, miti ya mazao,iko miti ya miiba, miti ya kunyonya sumu ardhini na mingine mingi. Ndivyo pia walivyo wanadamu. Wako sampuli tofauti, kwa madhumuni tofauti, kwa wakati tofauti. Muhimu ni kuwafahamu."
YapUkishusha utu na heshima ya mtu, unaweza jikuta umeudhi si yule tu uliyemlenga, bali na wale wanaomheshimu na kumthamini ambao wengine wanakumudu. Kabla hujamvaa mtu, pima ikiwa unammudu yeye na unamudu watu wake."