Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
KweliKatika maisha na haswa kwenye ushindani, jenga tabia ya kutowaacha wenzako mikono mitupu. Gawana ushindi, sifa au mafanikio na wengine kupunguza nongwa. Wakijisikia nao kushinda japo kiasi wanapunguza kukukamia kwenye ushindani ujao."
TrueKuishi ni kuegemeana. Kila mtu anatafuta egemeo na wa kumuegemea. Hata yule unayemuegemea na kupata amani ya akili na roho yako, naye kuna mahala kaegemea. Kabla hujaegemea, jiridhishe ikiwa unayemuegemea, anajua umemuegemea, naye kaegemea panapoegemeka. Egemea kwa tahadhari!"