Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Kwa walioulizia muegeya ndio huu hapa, wengine wanauita Mvunge.
images (1).jpg
images (2).jpg
 
Kwa walioulizia muegeya ndio huu hapa, wengine wanauita Mvunge.
View attachment 2276653View attachment 2276654
FAHAMU KUHUSU FAIDA ZA MTI WA MUINGE AU MUEGEA KATIKA TIBA ZA ASILI

MTI huu una majina mengi wengine huita muegea, muinge mlemela na majina mengine. Mti hutumika sana kukuzia maumbile ila kuna utaalam maalum hutumika ila nitawapa faida kiafya

KWA AFYA KWA UJUMLA

Unatibu Tumbo Kujaa Gesi Kujisaidia Milendalenda Vidonda Vya Tumbo Kunawirisha Mwili Kwa Wale Wenye Afya Mgogoro ukurutu na magonjwa mengine ya ngozi.

Jinsi ya kutumia Kupata faida hizo kwa kutumia mizizi ya mti huo, chukua mizizi au magome yake na uyakaushe kivulini (sio juani), baada ya kukauka, saga magome hayo ili upate unga. Chota unga huo kiasi cha gramu 700 (karibu na robo tatu kilo), changanya na maji kiasi cha lita 6. Mwenye tatizo anatakiwa kunywa mchanganyiko huo kwa kiasi cha robo lita kila siku

Hifadhi kwenye fliji ili isiharibike ukhtaj kutumia waipasha moto kidogo.

kukausha vidonda chukua unga huo hunyunyuziwa katika nguo au kitambaa na kisha nguo au kitambaa hicho hufungwa katika kidonda au jereha na baada ya siku kadhaa jeraha hilo hukauka.

KWA MARADHI YA WATOTO WADOGO

kupata tiba ya nimonia na matatizo ya tumbo ikiwa ni pamoja na minyoo kwa watoto, magome ya mvunge huchukuliwa na kulowekwa kwenye maji kisha mtoto mwenye tatizo la tumbo hunywesha maji hayo. Aidha, unaweza kutumia mizizi kama mbadala wa magome kutibu nimonia.

KWA WANAWAKE KUONDOA MAJI NA KUONGEZA JOTO NA HAMU YA TENDO LA NDOA

tafuta maua ya mti huo, huchemshwa au kukaushwa na kusagwa kisha huchanganywa na maji. Baada ya kupata dawa hiyo, muhusika anaweza kuitumia kwa kunywa kwa kipimo cha robo lita na nyingine kujisafishia sehemu za siri ndani ya ck saba mfululizo

pia mti huu hutumika kukuza maumbile kwa kuchanjia km inavyoelezwa na wengine wengi na pia kwa kupakaa baada ya kuandaliwa kwa kuchukua mti huu na kuchanganywa na miti na mafuta mengine.....
 
Kwani uzi mzima unaweza kufungwa kwa ajili ya comment za mjinga mmoja[mimi] si watanipiga ban tu.
Ndugu yangu hapana hapana hapana.

Wewe wasema lakini katu siwezi kuwaza wala kunena kuwa wewe huna uelewa, kwani mchango wako ni mkubwa sana kwa jamii na hata kwenye hili jukwaa.

Maoni yangu nimetoa tu kuulinda uzi huu lakini wadau wangeona hayana mashiko wangeyakataa pia. Ila wewe pia umeliona lina ukweli.

Tafadhali endelea kutusaidia wanajamii kwa elimu na uzoefu wako katika mpango wa afya zetu huku tukiulinda uzi wetu huu pendwa.
 
Kuna nko wangu alikua anasumbuliwa na kuwaka miguu moto..nilikua namuona anachemsha majani ya mimea flani..kisha anakanyaga miguu kwenye beseni lenye maji ya mimea hiyo..kiila siku asbuhi na usiku.

Alishaga pona kitambo..ngoja nitajaribu kuuliza ilikuwa na dawa gani.

#MaendeleoHayanaChama
Mkuu ukipata dawa nitag..mama yangu anasumbuliwa sana na miguu
 
TIBA YA FANGASI VIDOLENI
Osha sehemu yenye fangasi kwa maji ya moto kisha pakaa asali safi kila siku utapona
TIBA YA UGONJWA WA NGOZI
OSHA kwa maji ya moto sehemu iliyoathirika Na chukua mafuta ya habbatsauda changanya Na asali upake sehemu yenye ugonjwa
Kila Siku mpk upone
TIBA YA UGONJWA WA NGIRI
Juisi ya kitunguu thaumu ujazo wa chupa ya soda chemsha kwa nusu SAA mpk ibadilike rangi
Ikipoa kunywa vikombe2 vya kahawa kutwa mara3
TIBA YA MGONJWA MWENYE KIPINDUPINDU
Chukua vitunguu thaumu robo kg viponde Na mimina maji ya madafu vikombe viwili kisha umpe mgonjwa anywe vikombe vya kahawa 2 kutwa mara3 Tiba hii ifanye mpk apatapo nafuu au kupona kabisa
TIBA YA KICHOCHO
Juisi ya kitunguu thaumu kikombe kimoja Na uchanganye Na unga wa habbatsauda vijiko2 vikubwa koroga Na unywe nusu kikombe mara3 Kwa siku7mpk11 au21
TIBA YA UGONJWA WA TEZI
Majani mabichi ya mchungwa yaponde yalainike Na uponde vitunguu thaumu3 uchanganye changanya Na samli Na umfunge kwa bendeji kwenye tezi
TIBA YA MDUDU WA KIDOLENI
Chukua kitunguu thaumu kiponde kimoja mpaka kilainike nyunyiza kdg mafuta ya karafuu Na ufunge kwenye Mdudu
KUTOA GESI TUMBONI
Chukua Dawa inayoitwa shomari ujazo wa kijiko1 OSHA vzr tafuna kama karanga utapona.Kinga ni bora kuliko tiba.nimeicopy sehemu.
 
Nashukuru sana mkuu ntazingatia hilo nadhani ungenijuza mfumo wa dozi ingependeza zaidi pia, swali lilo ulizwa na mdau ni dawa ya asili ya kuondoa unene, nmeomba majibu kwakua kuna ndugu yangu pia anahangaika sana kutafuta dawa ya namna hiyo kwani amekua mzito sana hata kuanza mazoezi madogo madogo.
Mimi sio mtaalamu wa tiba ila niliweza kupunguza unene au uzito kwa kilo 20 ndani ya miezi 6 kwa kubalance vyakula yaani kula kwa kiasi. Baada ya kugundua chanzo cha unene au uzito ni chakula. Kuna baadhi ya vyakula kama sukari, sembe, soda niliacha kabisa. Wali, chapati za unga uliokobolewa, nyama, viazi nilipunguza kwa kiasi kikubwa kama matumizi niliyashusha hadi kufikia nusu na mengine robo. Hapa inahitajika nidhamu na uadlifu wa hali ya juu.

Wakati anasubiri kupewa mwongozo wa dawa au tiba azingatie utaratibu wa lishe hasa kuepuka vyakula vinavyoujaza mwili mafuta. Mtu aweza sema, sembe inaujazaje mwili mafuta? Tambua inaujaza kutokana na mifumo ya uchakataji na uhifadhi wa viini lishe mwilini. Ajitahidi kula mboga za majani na matunda.
 
Mimi sio mtaalamu wa tiba ila niliweza kupunguza unene au uzito kwa kilo 20 ndani ya miezi 6 kwa kubalance vyakula yaani kula kwa kiasi. Baada ya kugundua chanzo cha unene au uzito ni chakula. Kuna baadhi ya vyakula kama sukari, sembe, soda niliacha kabisa. Wali, chapati za unga uliokobolewa, nyama, viazi nilipunguza kwa kiasi kikubwa kama matumizi niliyashusha hadi kufikia nusu na mengine robo. Hapa inahitajika nidhamu na uadlifu wa hali ya juu.

Wakati anasubiri kupewa mwongozo wa dawa au tiba azingatie utaratibu wa lishe hasa kuepuka vyakula vinavyoujaza mwili mafuta. Mtu aweza sema, sembe inaujazaje mwili mafuta? Tambua inaujaza kutokana na mifumo ya uchakataji na uhifadhi wa viini lishe mwilini. Ajitahidi kula mboga za majani na matunda.
Nimekupata vyema kiongozi, niliwahi sikia funga pia ni tiba nzuri ya kupunguza unene.
 
wakuu kizunguzungu kinanitesa nimeambiwa tatizo ni kind ya vertigo
maana naona nakosa balance
 
Ndugu wanajukwaa wenzangu,ninawasalimu kwa jina la JMT! Kwa wale ambao Mungu anaendelea kuwajaalia afya njema basi ni jambo la kumshukuru Mungu,lakini pia kwa wale ambao wana matatizo mbalimbali ya kiafya si wakati wa kukata

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Msaada mkuu kwetu huku iyo miti haipo. Tunapateje hiyo Dawa.
 
Back
Top Bottom