Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

B, pamoja na kuwa na roho nzuri, una kila ishara ya kuwa na uwezo mkubwa wa akili. Umetoa ufafanuzi mzuri sana. Asante.
 
Akalale hostel za UDOM, Humanity/ social. Au aende COED, ng'hong'hona Au alale nanenane stand, mbona pazuri tu. Au aende uswahilini huko mailimbili nk
Na ukizingatia vikao vya kamati za bunge vimeanza, dodoma inafurika 😀😀🙌
 
Hii ni Makuna, naona kama iko vizuri.

Hii ni Pahi Hotel, nayo si haba.

Na hapa ni Kenya Lodge, pako vizuri kama Kenya kweli.

NB: Picha ni kwa msaada wa gugo, kama unafahamu sio nyumba sahihi naomba tupeane taarifa kuepusha kupotosha.
 
Akalale hostel za UDOM, Humanity/ social. Au aende COED, ng'hong'hona Au alale nanenane stand, mbona pazuri tu. Au aende uswahilini huko mailimbili nk
Na ukizingatia vikao vya kamati za bunge vimeanza, dodoma inafurika [emoji3][emoji3][emoji119]

Mkuu, hivi Hostel za UDOM huwa inawezekana wanaruhusu watu wa Saili kulala?

Kuna wazo hapa limenijia, hivi kwanini Chuo Kikuu UDOM kisingeanzisha utaratibu maalumu wa kuongea na Wanafunzi wao, ambao watakuwa tayari vyumba vyao vitumike kwa wanaofanya Saili kisha mapato yanayopatikana yawe ni sehemu ya ada yao ya Hostel na Chuo kipate kidogo!

Kuliko kuacha watu wateseke mitaani, naliona hili kupunguza sana gharama za wanaokwenda kufanya Saili na hata hao wanafunzi kupunguza au kuepuka kabisa kulipa ada za Hostel.
 
Wasiliana na uongozi wa chuo.
Na si. Udom tu, hata st John, CBE, nk.

Asante sana, nadhani kwa Dodoma Saili nyingi zinafanyika UDOM. Endapo kuna mahala unapajua Mkuu na ni pazuri kwa Saili za Utumishi Dodoma ila tofauti na zinazofanyika UDOM sio mbaya ukatusaidia pia.
Mimi huwa nikienda kifanya usaili Dodoma nalala lodge ya buku saba japo mazingira huwa ni magumu ila nakomaaa na ni karibu na Dom nauli huwa ni buku bajaji ukiwa unahitaji ni pm nikupe number zao hiyo lodge,,,saili zangu zote huwa nafikia hapo
 
Sawa Mkuu, naku PM. Asante sana.
 
Mimi huwa nikienda kifanya usaili Dodoma nalala lodge ya buku saba japo mazingira huwa ni magumu ila nakomaaa na ni karibu na Dom nauli huwa ni buku bajaji ukiwa unahitaji ni pm nikupe number zao hiyo lodge,,,saili zangu zote huwa nafikia hapo

Japo kwa faida ya wengine, nitaomba pia uniujulishe endapo itafaa tukiweka baadhi ya taarifa kuhusu hiyo lodge hapa hadharani watu wapate nafuu.
 
Boss Mungu akubariki sana, umetoa ufafanuzi mzuri sana. Nakutabiria hizi saili za mwaka huu, kuna moja wapo ni lazima itakuingiza kwenye ajira za Serikali.
Hahahaa, access ya mrija wa Asali kutokana na Tozo zetu tunaitafuta kwa udi na uvumba sana. Nchi ni yetu sote na keki ya Taifa ni haki ya kila mmoja wetu. Tupambane kwa njia yeyote tunayoona inafaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…