Ndugu
Mwifwa na wengine wote, asanteni sana kwa ule ushauri chanya, wakati mdogo wangu kwenye tangazo la kuitwa kwenye Usaili yupo lakini kwenye mfumo wa Utumishi akaunti yake ilikuwa kimya. Hatimaye ameona mabadiliko, na amepewa Namba pamoja na maelekezo ya venue.
Balaa liko kwenye ujasiri wa kwenda kuwania nafasi moja kati ya Sita miongoni mwa walioitwa 2455.
Japo kuna binti namfahamu, alipita na kupata kazi kwenye zaidi ya watu 1000 waliokuwa wanapigania nafasi 1 ya uhandisi na hana koneksheni wala pesa.