Mkuu, hivi Hostel za UDOM huwa inawezekana wanaruhusu watu wa Saili kulala?
Kuna wazo hapa limenijia, hivi kwanini Chuo Kikuu UDOM kisingeanzisha utaratibu maalumu wa kuongea na Wanafunzi wao, ambao watakuwa tayari vyumba vyao vitumike kwa wanaofanya Saili kisha mapato yanayopatikana yawe ni sehemu ya ada yao ya Hostel na Chuo kipate kidogo!
Kuliko kuacha watu wateseke mitaani, naliona hili kupunguza sana gharama za wanaokwenda kufanya Saili na hata hao wanafunzi kupunguza au kuepuka kabisa kulipa ada za Hostel.