Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

WAKUU SANA!

Magari yanayotembea usiku maarufu kama HAKUNA KULALA yanakamatwa kipindi hiki.... nyie mnaofanya USAILI tafadhalini sana.... usipange kuondoka usiku.... UTAKWAMA....!

CHUKUA HATUA

Kamanda Asante sana kwa msisitizo, naamini wengi tumejifunza kitu kupitia huu ujumbe wako.
 
Hello guys. Kwa wakazi wa Moshi kuna usafiri private kwa watu wanne interested.
Bei ni Tshs elfu 60 Go and return.
Tutaondoka jumapili tarehe 4/09/2022 saa moja asubuhi.
PACKAGE INCLUDES:
1.Usafiri kutoka Moshi bus stand saa moja asubuhi ya tarehe 20 hadi Dodoma mjini maeneo ya bunge.
2. Usafiri kutoka Dodoma mjini maeneo ya bunge hadi UDOM ukumbi wa CIVE au kumbi jirani saa kumi na mbili asubuhi (ili kuwahi interview).
3. Usafiri kutoka ukumbi wa interview hadi Dodoma mjini maeneo ya bunge tutakapofikia.
4. Usafiri baada ya matokeo kutoka ( approximately tarehe 6 au 7) kwa wale tutakaofaulu kwenda usaili wa mahojiano kutoka tulipofikia kwenda eneo la usaili wa oral(ofisi za bunge) kwenda na kurudi
5. Baada ya interview usafiri hadi Moshi stand. Kuanzia saa moja asubuhi (siku baada ya matokeo au second interview)
✓Other benefits include:
•Kudiscuss kwenye gari kwa pamoja
•Kusimama popote njiani and other benefits of a private travel.
DM if interested.
MALIPO YANAPOKELEWA KWA MKONO MWISHO SIKU YA JUMAMOSI YA TAREHE 03/09/2022 SAA SITA MCHANA

Aiseee hii nimeipenda sana, kama ingekuwepo na kwa watu wa Dar es Salaam ingependeza sana.
 
Asante sana Mkuu, samahani kwa swali la ziada kwa sasa nauli ya Dodoma kwa wastani ni kama kiasi gani? ...
Nauli ya chini kabisa ni 25K, Luxury unapigwa hadi 30K.

Niliwahi kupanda Chiloha nilikuwa natokea Dom kuja Dar, niliambiwa 30K nikagoma nikasema nina 25K wakachukua
 
Nauli ya chini kabisa ni 25K, Luxury unapigwa hadi 30K.

Niliwahi kupanda Chiloha nilikuwa natokea Dom kuja Dar, niliambiwa 30K nikagoma nikasema nina 25K wakachukua

Asante sana Mkuu.
 
Asante sana Mkuu.

Hapana, anayeenda kufanya sio mimi. Japo na dogo analalamika necha ya mahitaji ya kazi inamfanya ashindwe kutabiri mtihani wa Usaili unamhitaji aandae nini.


Namimi nimepitia ni kweli Mkuu, tofauti na mtu kuvujishiwa mtihani, nina uhakika nafasi ya Katibu Msaidizi wa Bunge Daraja la II hakuna mtu mwenye uhakika wa anachojiandaa nacho. Wengi watapigwa na butwaa kwa watakachokikuta.

Afadhali taaluma nyingine uwezekano wa kubashiri upo, na ni mkubwa.
 
Usaili wa kitu gani
Wakuu mambo vipi? Naona ma PDF yameanza kumwagika, changamoto ya malalamiko ya kwanini Utumishi wako kimya, inakwenda kuisha huku changamoto nyingine zinazotokana na kuitwa zinaanza kuibuka kwa kasi ya ajabu. Hii ni kwa wote, wanaokwenda kwenye Saili mbalimbali na hata wanaowategemea.

Tafadhali, naomba tutumie uzi huu kwa kutaja, nyumba za wageni ambazo ni rahisi mtu kukaa na kufika eneo la Usaili kwa gharama ndogo, maeneo zilipo, gharama na hata mawasiliano kama yapo. Hii itasaidia wengi hasa wanaokwenda kwenye Saili Dodoma kwa mara ya kwanza, au hata waliowahi kwenda na wakaishia kuteseka.

NB: Japo sio kwa umuhimu, inasemekana wengine hulala nje, baa na maeneo mengine kwa kutokuwa na pesa kabisa. Kama hayo maeneo yapo na ni salama naomba tusaidiane kuyataja ili watakaojikuta hali haziruhusu wakimbilie huko.

Asante.
 
Back
Top Bottom