Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

huyo hajabobea vya kutosha, kubobea vya kutosha ni hadi ufanye super specialization i.e PhD (Doctor of Philosophy ).

Sawa Mkuu, asante sana kwa ufafanuzi. Nadhani pia tukiiweka kwamba nilidhamiria inaweza kuwa ni yeye au wengine wamo humu waliobobea inaweza ikaleta mantiki.
 
Wakati tunaendelea kuchangamsha uzi, ili wanaotafuta sehemu za kulala kwenye Saili waukute kirahisi, wakuu nimegundua kwa mtu anayelenga kuajiriwa kwa programu tofauti na za Sayansi ajikite kusoma Business Administration, yani hii kitu kwenye nafasi zinazotangazwa karibu zote wanaruhusiwa kuomba.

Hata za ulinzi hawa jamaa wanapewa nafasi. Hii sijui imekaaje, wakati kuna wengine kozi zao wanabanwa sana, hawawezi kuomba tofauti na walichosomea moja kwa moja!
 
Kweli mkuu hiyo kozi ni universal, hasa ukiisoma Masters unakuwa na uwanja mpana wa kuiendea Asali
 
haina issue hiyo, kozi zenye maslahi ni MD,PHARMACY,NURSING, UPIMAJI ARDHI,USANIFU MAJENGO,
Kuna jamaa ni Surveyor naona mambo yake sio mabaya, ameingia kwenye mrija juzi kati kupitis PSRS.

Kabla ya hapo jamaa alikuwa kwenye maproject mbali mbali na tayari alikuwa kashaseti mambo yake vizuri hapa mjini ikiwemo tayari kashasimamisha mjengo imebaki finishing tu ahamie.
 
Kuna Lodge inaitwa Galilaya,iko kisasa kule.mimi huwa nikienda Dom huwa nafikia huko.bei yake ni 15,000/=haina maji ya moto.asubuhi wanatoa chai mkate na yai moja.binafsi me naona iko vizuri tu.mnaweza mkaitafuta tu vijana.
 
haina issue hiyo, kozi zenye maslahi ni MD,PHARMACY,NURSING, UPIMAJI ARDHI,USANIFU MAJENGO,

Ni kweli Mkuu, kwa upande wa masilahi uko sahihi sana. Ukija upande wa pili, kwa anayelenga ajira za Serikali ndipo changamoto ilipo. Business Administration ana wigo mpana wa kuomba idadi kubwa ya kazi zinazotolewa kuliko hizo ulizo orodhesha, au unaonaje mkuu?
 
Kuna Lodge inaitwa Galilaya,iko kisasa kule.mimi huwa nikienda Dom huwa nafikia huko.bei yake ni 15,000/=haina maji ya moto.asubuhi wanatoa chai mkate na yai moja.binafsi me naona iko vizuri tu.mnaweza mkaitafuta tu vijana.

Mkuu asante sana kwa kutujuza, binafsi nimeipenda sana. Hasa hapo kwenye kutoa chai mkate na yai.

Vipi kwa asiyewahi kabisa kufika Dodoma anaweza kutamani kufahamu, kutokea ilipo Galilaya lodge ni gharama kiasi gani kufika eneo la usaili UDOM na je umbali unaruhusu kuwahi saili za mapema?

Natangulisha shukurani.
 
Ni kweli Mkuu, kwa upande wa masilahi uko sahihi sana. Ukija upande wa pili, kwa anayelenga ajira za Serikali ndipo changamoto ilipo. Business Administration ana wigo mpana wa kuomba idadi kubwa ya kazi zinazotolewa kuliko hizo ulizo orodhesha, au unaonaje mkuu?
hizo ajira za bussines admini si ndio zile nafasi 10 watu 2000
 
Hahaha, ndio hizo Mkuu. Kizuri kila PDF wana nafasi zao, ukiacha zinazohitaji watu wa Sayansi.

Lakini zile programu ngumu ngumu ndio nyingi zinataka watu wachache sana, na zenyewe kutoka ni adimu unaweza pishana na PDF nyingi sana haziwahitaji, kizuri ni ukipata umetusua.
 
Upo sahihi sana yani haya makozi yetu magumu unaweza kukaa mwaka mzima ikatoka nafasi moja tu ,wakati huo unakuta kozi za business kila siku zinatoka
Hahaha, ndio hizo Mkuu. Kizuri kila PDF wana nafasi zao, ukiacha zinazohitaji watu wa Sayansi.

Lakini zile programu ngumu ngumu ndio nyingi zinataka watu wachache sana, na zenyewe kutoka ni adimu unaweza pishana na PDF nyingi sana haziwahitaji, kizuri ni ukipata umetusua.
 
Mkuu asante sana kwa kutujuza, binafsi nimeipenda sana. Hasa hapo kwenye kutoa chai mkate na yai.

Vipi kwa asiyewahi kabisa kufika Dodoma anaweza kutamani kufahamu, kutokea ilipo Galilaya lodge ni gharama kiasi gani kufika eneo la usaili UDOM na je umbali unaruhusu kuwahi saili za mapema?

Natangulisha shukurani.
Kutoka kituoni mpaka ilipo ni mwendo wa kutembea kwa miguu kwa dakika zisizozidi tano tu.
Kutoka kisasa mpaka udom unaweza ukachukua daladala zinazotoka nanenane kwenda udom au ukaenda mpaka sabasaba ukachukua daladala zinazoelekea udom.kama mfuko unaruhusu unaweza chukua boda mpaka udom ni elfu 5 tu.
 
Upo sahihi sana yani haya makozi yetu magumu unaweza kukaa mwaka mzima ikatoka nafasi moja tu ,wakati huo unakuta kozi za business kila siku zinatoka

Ni kweli kabisa Mkuu, asante.
 
Kutoka kituoni mpaka ilipo ni mwendo wa kutembea kwa miguu kwa dakika zisizozidi tano tu.
Kutoka kisasa mpaka udom unaweza ukachukua daladala zinazotoka nanenane kwenda udom au ukaenda mpaka sabasaba ukachukua daladala zinazoelekea udom.kama mfuko unaruhusu unaweza chukua boda mpaka udom ni elfu 5 tu.

Sawa Mkuu, asante sana. Naamini wengi watafaidika na hii taarifa yako.
 
Wadau mpo kimya kulikoni.

Updates za accomodations za gharama nafuu zimeisha?
 
Back
Top Bottom