Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

Dogo atakuwa kashakandwa huyo, tuombe asivurugwe na kusahau hizo chimbo za lodge[emoji3][emoji3][emoji3]

Hahaha! Aisee amefanya mtihani wa NAOT alipotoka nikamuuliza atabaki kusubiri matokeo ili aingie Oral au atarudi, akanijibu kwa mtihani ulivyokuja ni bora aokoe pesa kwa kuwahi kurudi nyumbani mapema, eti hana muujiza wa kuusubiri.
 
siku Bado nyingi mpaka tr7 Bora walivyorudi kwao kwanza

Kabisa Mkuu, maana kuishi lodge na kulipia gharama za kujikimu kila siku mpaka watakapotoa matokeo ni risk sana. Unaweza jikuta umepoteza pesa nyingi sana.
 
Jina: Melisa lodge

Eneo: Majengo

Mawasiliano: 0762 682 121

Gharama: Vyumba vyote bei ni Tzs 15,000/=

Kwa taarifa niliyopewa, pako vizuri sana, eneo halina kelele, pasafi, usalama upo na wahudumu ni wakarimu.
 
Majengo ipo sehemu gani?
 
Hahaha! Aisee amefanya mtihani wa NAOT alipotoka nikamuuliza atabaki kusubiri matokeo ili aingie Oral au atarudi, akanijibu kwa mtihani ulivyokuja ni bora aokoe pesa kwa kuwahi kurudi nyumbani mapema, eti hana muujiza wa kuusubiri.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupiga pepa ya PSRS?
 
Ipo maeneo yale ya sabasaba kwa mbele tu kidogo unatembea au kama anaijua ofisi ya tanesco ni hapo hapo
Namimi sina wenyeji sana na Dodoma ila haiko mbali sana na stendi ya sabasaba. Hiyo (Majengo sokoni) ndiyo mitaa ya kina msanii Monicentral zone.
 
Hivi ule mpango wa kufanya usaili angalau kwa kila mkoa , au kila kanda umeishia wapi, au ndio mambo ya Bajeti kutokutekelezwa.

Nchi ya hovyo sana hii
 
Ipo maeneo yale ya sabasaba kwa mbele tu kidogo unatembea au kama anaijua ofisi ya tanesco ni hapo hapo

Ohooh, sawa Professor. Kumbe unapajua? Au uliwahi kufikia hapo nini?
 
Hivi ule mpango wa kufanya usaili angalau kwa kila mkoa , au kila kanda umeishia wapi, au ndio mambo ya Bajeti kutokutekelezwa.

Nchi ya hovyo sana hii

Hahaha, Mkuu hii nchi kwa sasa tujipambanie wenyewe na watu tunaojuana nao. Tofauti na hapo utaambiwa uhamie Burundi.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupiga pepa ya PSRS?

Hahaha, huu ni wapili Mkuu, ila wakwanza ulimjia vizuri na akawa na matumaini makubwa mpaka matokeo yalivyotoka ndipo akagundua utumishi hawaishiwi mbinu za kumshangaza jobless.
 
Back
Top Bottom