Victoire
JF-Expert Member
- Jul 4, 2008
- 24,386
- 57,588
Wewe acha uongo. Watu wapo wengi tu.Nipo kwenye mkutano hapa na nimefika muda mrefu sana ili kusikikiza sera mbadala kutoka kwa viongozi wetu na mgombea wetu.
Kabla ya yote jana mgombea wetu alitueleza kuwa tutafanya maandamano ya amani kabla ya mkutano kuanza ila ukweli ni kuwa hatujafanya maandamano hadi sasa na tupo hapa hatujui kinachoendelea.
Watu tupo wachache kuliko jana mbagala, ila hii inaweza kuwa bahati mbaya kwa sababu nadhani wamechagua sehemu ambayo haikuwa sahihi.
Kawe ni sehemu ambayo imezungukwa na sehemu za ushuani ambao huwa hawapendi kabisa mikutano ya kisiasa. Ningekuwa mimi huu mkutano leo ungefanyika ubungo, magomeni au kimara lingetafutwa eneo zuri la wazi maeneo hayo kwa ajili ya mkutano.
Ila yote kwa yote kuna shida ndani ya chama.