Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halafu wanauza bei ya kutupa washenzi wale...mmfano kiatu jumla kinauzwa 3200 ye anatoka nacho nje anauza 3500. Ana hasara gani..anauza piece hamsini kwa siku halipii chochoteSwala la machinga waondoke tu mjini wanaua biashara watengewe maeneo yao Magufuli alibugi sana
Kwanza hawalipi kodi na wanaponunua bidhaa hawaombi risiti kwenye maduka makubwa so serikali inapata hasara ya kodi.
Vile vile wengi mjini ni wafanya biashara wakubwa wanafanya kutoa pesa kwenye mfuko wa suluali na kuweka kwenye mfuko wa shati.
Ndio maana ukwepaji kodi unaongezeka kwa sababu watu wenye address za kulipa kodi biashara zao wanachukua machinga.
Halafu machinga wenyewe wanauza sana halafu hawana leseni za biashara za kufanyia kazi wengine unakuta ndio wale waliofunga maduka kipindi cha Magufuli unakuta machinga ameweka bidhaa za milio 10 nje hii sio haki hata kidogo.
Watafutiwe maeneo maalumu kama Tandika tegeta, Ubungo mbagala wawe na shopping mail zao na walipe kodi ili tuone kama watauza tens bidhaa ovyo na kuhatarisha hata maisha ya wanunuzi.
Unakuta mtu anauza nyanya kariakoo katikati ya barabara seriously sehemu ambayo mnasema ni soko la kimataifa.?
Si nje sana,angalia sasa hivi mbagala mwisho pale au tandika kushakua full,lile shazi sasa hivi linahamia mbezi na tegeta nyuki huko,sasa maeneo kama hayo kama yanaandaliwa ipasavyo baada ya miaka kadhaa watu watazoea huko nje ya mji na pale town patamua kimtindoSasa nje ya mji wakati wao target yao ni wale watu wanaopita pita stand
... "maeneo yasiyo na tija"; hapo ndipo tatizo lilipo! Kwao maeneo yenye tija ni maeneo yenye "watu wengi" na maeneo yenye watu wengi obviously ni katikati ya miji na pembezoni mwa barabara kuu kuingia mijini.Tayari wameshatafutiwa au watoke kwanza,
MAANA kilio chao toka zamani ni kuwa maranyinhi huwa wanapelekwa au kutengewa maeneo yasiyo na tija kwa biashara zao
Duh sijui itakuwaje
Katika mambo nitakayo muunga Mkono Mama ni hili la wafanya biashara wa vibanda mitaani, waondolewe, na kama wawepo ni kwa utaratibu maalumu na wawe na efd machine au wafuate utaratibu wa Rwanda kuwa sehemu moja .Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.
Watafutiwe sehemu salama kwa ajili ya biashara zao.
Wavunje sheria Kisa wamechukua mikopoHao wanaotolewa maeneo hayo wanatarajiwa kuhamishiwa wapi?. Mtihani mpya kwa wale waliochukua mikopo haswa kina mama wanaotegemea vikoba na pesa za aina hiyo.
Karume biashara ipo sababu sehemu imepakana na highway na kituo cha dala dala! Mbali na hivyo pako level moja yani tambarare kiasi kwamba mtu anaweza maneuver eneo lote bila hussle!Nadhani kama taifa lazima kuwa na utaratibu maalum, haiwezekani watu wanaamua kufanya kila sehemu ni ya kuuza matango, parachichi, chupi, blauzi Yani vurugu tupu.
Serikali imetenga maeneo ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo masoko, viwanja vya magulio ya wiki, minada, viwanja vya mpira, na kila aina ya shughuli mbalimbali Zina maeneo yake.
Kitendo cha machinga kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi inakosesha Halmashauri mapato ya ushuru pamoja na Kodi za pango. Pia tunakuwa tunawaumiza wale walioweka biashara zao maeneo rasmi na hii ni double standard haifai kama taifa.
So walizoea kuwekwa maeneo yasiyo rasmi na ilikuwa kuna kero zake na raha yake pia Ila hata mie naona waondoke tu waende sehemu rasmi.
Hapo zamani tulishazoea mtumba ni Karume tu baada ya manzese kutimuliwa Ila sasa najiuliza wale walioenda Karume so hawapati biashara? Hii sio sawa. Warudi kule.
😆 serikali ndo ilikuwa inapoteza.Sasa hii si ndio ilikuwa tamu zaidi mkuu maana hamna ku file taxes😂😂😂
Sasa nani anataka kuifanyia kazi serikali mzee! Mi nilipe kodi ili wapuuzi wachache wanaolipwa posho za laki 3/3 kilasiku wakajadili kurasimisha gongo na kutuchangisha shilingi 50 kila siku kwenye simu?😆 serikali ndo ilikuwa inapoteza.
🤣🤣🤣🤣Watakuja kusema"baba yetu kaondoka sasa wanatunyanyasa"
Kabisa, mfano serikali inajenga barabara kurahisisha usafiri, sasa mfano ukienda mbagala, tegeta, bunju B kunakua na foleni kisa vibanda vinasababisha parking kua finyu na daladala kupaki barabarani.Hivi hoja za ajabu kama hizi mnazitoa wapi? Nchi ifike mahali raia wafuate sheria , Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma, iweje sasa raia wengine Sheria iwe butu kwao kisa machinga? Raia kama hana shughuli ya Msingi ya Uzalishaji mjini kati anafanya nini? Warudi kwenye kilimo nchi ipate uchumi kukua, hii ya kufanya uchuuzi Nchi haifaidiki chochote kwa hawa raia wachuuuzi.
Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Endelea kuwapa kichwa nakukumbusha tu mgambo wa Jiji ni Vijana wa JKT mtapigika kipigo Cha mbwa kokoDah kwahio waondolewe road reserve tu mkuu ila wabaki mbele ya maduka!?