Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,404
- 10,900
Tunarudi kijijini kulimaSiyo wanahamishwa, wanaondolewa kwa kwenda watajuwa wenyewe.
Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunarudi kijijini kulimaSiyo wanahamishwa, wanaondolewa kwa kwenda watajuwa wenyewe.
Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Kumbe ni vibanda tu na wataendelea kuwa kero!!!!View attachment 1780963
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amewataka wafanyabiashara waliojenga vibanda katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuviondoa kabla ya Mei 18, 2021.
Wakati Shauri akieleza hayo, gari lenye spika za matangazo linapita katikati la mitaa ya Jiji hilo likitangaza kuhusu mchakato huo kwamba vibanda havitakiwi kuonekana kando ya barabara.
Akizungumza na Mwananchi Digitial leo Jumanne Mei 11, 2021 Shauri amesema hawajazuia wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao, wanachotakiwa kufanya ni kutojenga vibanda na kuwataka wauze bidhaa zao kwenye meza ili wakimaliza iwe rahisi kuziondoa na kuacha maeneo wazi.
Amebainisha kuwa sheria ya mipango miji hairuhusu kujenga vibanda, kuwataka wafanyabiashara hao kutii agizo hilo.
“Mwisho Mei 18 kama ambavyo gari la matangazo linavyotangaza waviondoe vibanda vyao kwa sababu vingine vinajengwa hadi kwenye njia za watembea kwa miguu na barabarani na kuleta adha kwa watumiaji. Wanatakiwa watii sheria bila shuruti waviondoe wenyewe,” amesema Shauri.
MWANANCHI
Kariakoo barabara ya Msimbazi nafikiri wameigawana ni sisi tu hatujui...watembea kwa miguu hatuna chetu..Nimetoka tu nje ya ofisi nikakutana na gari ya tangazo inaanza kutangaza, watu wameshika vichwa wengine wanacheka na mimi ikabidi nicheke.
Ila wametubana sana watembea kwa miguu aisee
Dar ndio wapi? Mbezi Luis inatia kinyaa mabanda mpaka mitaroni huko wameruhusiwa kujenga mabanda mitaro ya maji?Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es Salaam...
Mkuu kweli Mbezi Luis imezidi mno kwa uchafuzi wa mazingira nadhani hali hii imechangiwa na uwepo wa Magufuli Bus Stand. Ile Stand ya daladala kuanzia saa 12 jioni inageuka na kuwa soko, nawahurumia sana wahudumu wa ufasi.Dar ndio wapi? Mbezi Luis inatia kinyaa mabanda mpaka mitaroni huko wameruhusiwa kujenga mabanda mitaro ya maji?
Hebu na wasafishe jiji letu