Hakuna cha kuingizwa chaka hapa. Hakuna mtu anayesema dini ya Israeli ni Ukristu. Kinachosemwa ni kwamba Kristu alikuwa Myahudi aliyezaliwa huko huko Israeli. Taifa lake mwenyewe walimkataa hadi wakamuua. Alidiriki hata kusema 'nabii hatambuliki kwao'. Kutambua mtu na kutambua nchi anakotoka ni vitu viwili tofauti. Kwa mfano kabla ya mwaka 1994 wakati Mandela alipokuwa bado gerezani, kuna watu wengi waliokuwa wakimtambua (pamoja na Serikali ya Tanzania) lakini walikuwa hawakubaliani na Serikali ya nchi yake ya Afrika ya Kusini. Yesu aliyeanzisha Ukristu, alizaliwa Bethlehemu huko Israeli. Maria, mama yake, na Yosefu, baba yake mlishi, walikuwa raia wa Israel. Aliteswa huko Kalvario, akatundikwa msalabani Golgota hadi akafa na kuzikwa huko. Wafuasi wa dini aliyoanzisha hawawezi kuacha kwenda kuzuru maeneo hayo eti kwa sabababu tu serikali yake hawakumkubali. Ni kweli kwamba takriban asilimia 85 ya watu wa Israeli dini yao ni Judaism na chini ya asilimia 5 ndiyo Wakristu, wanaomfuata mzawa wa huko Uyahudini. Wao walimkataa wakadiriki hata kumuambia Pilato, mkoloni wa Kirumi, kwamba wao wanamtambua Kaysari wa huko Roma, na siyo huyu mtoto wa nyumbani. Mtawala wanayemtambua ni huyo mfalme wa Roma.
kwa ufupi, tutenganishe kumfuata mtu na kufuata sera za serikali ya nchi yake.