macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 29,500
- 61,451
Huu ni ujinga wa hali ya juu. Unamlaumu Nyerere aliyefariki miaka mingi iliyopita? Kwanza ujue wakati wa Nyerere hakukuwa na ujinga wa namna hii. Yaani kipindi cha Nyerere kiongozi au mfanyakazi wa serikali awatambie wananchi eti anatumia vitu vya gharama? Tatizo ni wananchi wa Tanzania ambao wengi wana mawazo ya kupenda vya kuletewa kama wewe. Umekaa kibarazani ukisubiri watawala wakuletee mfumo mzuri! Kwa taarifa yako: nchi zote unazoziona zenye mifumo mizuri, hiyo mifumo haikujileta yenyewe. Na wala siyo watawala waliyoileta. Ni wananchi walikuwa wakali na kuungana kuondoa mifumo mibaya.Haya ni matunda ya mfumo mbovu alioujenga Nyerere