Video Clip: Jerry Silaa adai kuna Jaji anamlinda tapeli wa viwanja

Video Clip: Jerry Silaa adai kuna Jaji anamlinda tapeli wa viwanja

Huyo Jaji muda si mrefu atatimuliwa, na uhakika kwa uongozi makini wa Mama yetu Samia, hatuwezi kuwa na Jaji anatumia taaluma yake kulinda matapeli, ukiona hiyo huyo Jaji ni mla rushwa mkubwa sana na uhakika ataondolewa haraka sana
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Hapana!! Sio kuingilia mhimili wa, mahakama. Amesema ukweli. Huyo Jaji atatumiwa kimemo na Rais ili ajiuzulu mwenyewe. Hawaii kuwa, pale. Ni mla rushwa mkubwa. Wakati wa, JPM kuna, majaji walikula rushwa. Walitumiwa vimemo vya kujiuzulu. Na wakafanya hivyo.
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Hapana...corruption imepitiliza. Tatizo letu kubwa ni kufikiri ukipewa kazi za umma na vyeo basi uko special. Hata kama wanyonge wanaumizwa, asiguswe mtu.
Sio sawa. Lets go to the basics
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Muhimili wa mahakama ni mchafu sana pia. Mzee wangu aliporwa haki yake na jaji wa mahakama kuu na historia inaonyesha aliwekwa hapo na hayati JPM ni msukuma mwenzake na hakuwa vizuri kwenye fani husika.

Mahakama ni tawi tu la CCM, lina uchafu mwingi sawa na mihimili mingine.
 
Shamba la bwana ISSA, mbuzi wa bwana ISSA...... Watajuana wenyewe
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Kwahiyo kama ni Kweli akae kimya?

Nchi yetu ianamalizwa na wasomi na watu wanaojidai wajuaji

Eiishhh
 
Awali "Y" alikuwa Wakili na aka attest nyaraka za Mzee "X". Hatimaye Tapeli "Z" akadhulumu kiwanja, kesi ikafunguliwa. Na kwa bahati mbaya ikaanguka kwa Jaji "Y" ambaye ndiye alikuwa Wakili wa Mzee "X". Na sasa Jaji "Y" anawaita Mawakili wa Serikali kutaka kuwa CORRUT.

Je huyu Jaji "Y" ni nani? Na Je huyu Tapeli "Z" ndiye Alex Msama au Mushi?

Haya wataalamu wa mambo ya ARDHI tufungulieni codes.
---
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuwa ameandika barua kwenda kwa Waziri wa Katiba na Sheria kufuatia jaji mmoja wa mahakama kukiuka kanuni za taaluma.

Waziri Silaa akihitimisha hoja ya bajeti yake bungeni amesema kuwa mwaka 2015 jaji huyo alikuwa wakili, na akamsaidia tapeli mmoja kuchukua ardhi ya watu.

Amesema warithi wa aliyetapeliwa walipoenda makamani hivi karibuni, wamekuta wakili yule sasa ni jaji, bado akaamua kwa kumnufaisha tapeli.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, na kwamba jambo hilo amelichukua yeye ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na haki inapatikana.

Credit: TBC
Jerry ni LLB, imekuwaje afike mbali hivi na kutoa tuhuma kubwa namna hii bila kusikiliza pande zote mbili? anayesemekana kuwa tapeli alipoongea kwenye clip yake mbona kama hoja zake zina mashiko?

kuna kitu kimoja tufahamu, kati ya vitu unatakiwa kuogopa wewe ambaye pengine umefanikiwa maishani, ni kugombana na mtu wa hali ya chini. kuna wafanya biashara, kuna wafanyakazi wa umma au matajiri, huwa wanapoteza sana haki zao mbele ya watu wa hali ya chini kwasababu kiongozi yeyote hasa hawa wa kisiasa akiwaangalia, anaamini lazima wewe mwenye uwezo utakuwa unamuonea na anakuwa biased against you kwasababu tu una kipato. ndio maana tunahitaji chombo kilicho katikati bila kuwa biased, na Mahakama hata ikilalamikiwa vipi ndio chombo cha katikati, kila mtu alete hoja zake na mahakama iamue. huna hoja umepoteza. nilishawahi kupitia mazingira kama hayahaya tena kwenye mambo ya ardhi kama haya,mtu mmoja wa hali ya chini ameenda kulalamika hadi kwa waziri huko ati namwonea, nilipambana na kwa msaada wa Mungu ikaja kugundulika kumbe yule mtu wa chini ndio alikuwa mwongo na tapeli akitumiwa na watu wengine wenye pesa kupora ardhi yangu ili wafaidike pamoja. hapa ndipo nilipojifunza sio kila unayekutana naye analia ameonewa, wengine huwa wanalia kwasababu wamekwamba kuonea wengine, wamekutana na saizi yao.
 
Mahakama ichunguze, kama hii tuhuma haina mashiko, itoe tamko kali. shida hawa wanasiasa huwa wanaamini hawatakuja kutoka madarakani na siku zote huwa wanakuwa upande wa yule wanayeamini anaonewa kumbe pengine huyo ndiye anaonea tajiri. mtu kawekeza pesa yote hiyo, na nyaraka anazo, ungekuwa wewe ungefanyeje?
 
Jaji kama huyo unamfanyaje Sasa???.

Ndio sababu PAUL MAKONDA, ANAPENDWA KAMA ALIVYOKUA MAGUFULI.

Nchi hii Kwa Sasa tuna

Makonda.... Silaa, Mpina....Mchengerwa...Msambatavangu.... Gwajima..Gwajima Ke, Bashungwa ,

Bado tuna watu bado tunao.
mchengerwa?
huyu mkwe wa samia?
hauko serious mkuu
 
Back
Top Bottom