VIDEO: Hili lilimshinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete hata Magufuli. Rais Samia apongezwe

VIDEO: Hili lilimshinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete hata Magufuli. Rais Samia apongezwe

Aliienga kwa aslimia 15% na alonenga kwa asilimia,85% ni nani wa kumsifu?
Kunenga ndo nini mkuu?

Unahisi mama Samia alikuwa na choice kwa hali ilivyokuwa na status ya mradi ulivyokuwa umefikia?

But sijui hata tunabishana nini wakuu, kwani akijenga JPM na akijenga Samia what is the difference kwa watanzania? Hii ndio shida ya nchi kutokuwa na vipaumbele kama Taifa, kila kitu kinafanywa kwa matakwa ya Rais aliyepo madarakani matokeo yake mnaona kama anawafanyia favour

Ujinga mtupu.
 
Hakuna mradi wowote ulioanzisha na Miss Deaf Frog, kila alichokimalizia kilishawekewa misingi na Magu.

Alivyoasisi Frog ni kuuza vitu, kupandisha gharama za maisha na kuhudhuria kila mualiko duniani kama Mc wa shughuli.

Bila ya miradi iliyoanzishwa na Magu Chura angebakiwa na nakala ya Movie yake ya wanyama pori kama Tarzan.
Ifahamike pia kuwa hiyo movie ya Tarzan raia wameshaisahau kabisa
 
Lakini hebu tuwe wakweli mtu kachukua mradi ukiwa 35%,

Hivi unajua hii hata nusu ya Mradi ilikuwa bado?
Ishu hapa ni ujasiri wa kuasisi hiyo miradi.
Mama ameshaasisi nini cha maana so far?.
Kama chuma kingekuwa hai kingekuwa na hii miradi aliyoiacha tu mpaka leo? Kuuza rasilimali kwa kigezo cha uwekezaji ni kukusa ujasiri na ubunifu wa miradi mipya na kutoamini watu wako.
 
Uongo mbaya, Samia kajitahidi sana kukamilisha miradi ya kimkakati ya Magufuli. Kama asingekomaa vya kutosha bwawa la Umeme la Stieglers lisingekamilika na Reli ya SGR isingepata push ya kutosha.

Hata ndege ameendelea kuleta nyingi tu!

Apewe maua yake!

Bi Mkubwa popote ulipo pokea pongezi kutoka kwangu ( Missile of the Nation) ila sasa:

1. Acha kuingia mikataba mibovu ya kugawa rasilimali za nchi kama vile ardhi, bandari, misitu etc

2. Punguza safari
3. Zuia mara moja mambo ya wasiojulikana yaliyoanza kurejea, yanakuchafua.
4. Tuletee katiba nzuri ili iwe ni legacy yako bora
Mama ni kiongozi mzuri sana sema kila siku nasema shida iko kwa alio waamini wapige kazi ndo wanamwangusha sana tena sio kidogo.Wanakuja na stori za mama anaupiga mwingi kumsifia kinafiki uku wanamwangusha na kumpaka matope.Mama kama angepata watu kumi km makonda sidhani hata kama tungekua tunapiga kelele.
 
Tunaweza kubishana juu ya mambo mengi ila hatuwezi kubishana juu ya utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo unaofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mtakubaliana na Mimi kuwa Mradi huu uliwashinda akina Mzee Julius Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete hata John Pombe Magufuli wakati anafariki akiwa madarakani kwa miaka zaidi ya mitano aliutekeleza kwa 35% tu,

Maajabu ni haya, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka mitatu tu kazi IMEKWISHA mnadhani kwanini Watanzania tusimpongeze Mama na kumtia moyo kuelekea 2030?​
Samia mwamba sana hapa Duniani kwa hekima na akili nyingi
 
Mama ni kiongozi mzuri sana sema kila siku nasema shida iko kwa alio waamini wapige kazi ndo wanamwangusha sana tena sio kidogo.Wanakuja na stori za mama anaupiga mwingi kumsifia kinafiki uku wanamwangusha na kumpaka matope.Mama kama angepata watu kumi km makonda sidhani hata kama tungekua tunapiga kelele.
Sahihi hawa wengi wao si waaminifu
 
1. Umeme ni Magufuli
2. SGR ni Magufuli
3. Kuuza Bandari Samia
4. Kuuza KIA Samia
5. Kuuza Misitu Samia
6. Kuuza Ngorongoro Samia
7. Kuuza Ardhi ya Tanganyika Samia.

Mengine yote porojo.
Tuna dili na viumbe hai ...miaka 3 ya samia imeonyesha uwezo wake
 
Uongo mbaya, Samia kajitahidi sana kukamilisha miradi ya kimkakati ya Magufuli. Kama asingekomaa vya kutosha bwawa la Umeme la Stieglers lisingekamilika na Reli ya SGR isingepata push ya kutosha.

Hata ndege ameendelea kuleta nyingi tu!

Apewe maua yake!

Bi Mkubwa popote ulipo pokea pongezi kutoka kwangu ( Missile of the Nation) ila sasa:

1. Acha kuingia mikataba mibovu ya kugawa rasilimali za nchi kama vile ardhi, bandari, misitu etc

2. Punguza safari
3. Zuia mara moja mambo ya wasiojulikana yaliyoanza kurejea, yanakuchafua.
4. Tuletee katiba nzuri ili iwe ni legacy yako bora
Hapo umeongea kama mtanzania ..hawa kenge wengine wanaongea kama wao ni wana siasa
Mambo ya siasa tuwaachie wenyewe sie tufocus na maendeleo anayofanya na anapokesea tunapaza sauti na sio kuleta matuc kama sativa
 
Tunaweza kubishana juu ya mambo mengi ila hatuwezi kubishana juu ya utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo unaofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mtakubaliana na Mimi kuwa Mradi huu uliwashinda akina Mzee Julius Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete hata John Pombe Magufuli wakati anafariki akiwa madarakani kwa miaka zaidi ya mitano aliutekeleza kwa 35% tu,

Maajabu ni haya, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka mitatu tu kazi IMEKWISHA mnadhani kwanini Watanzania tusimpongeze Mama na kumtia moyo kuelekea 2030?​
Mimi ningeiweka hivi. Kila awamu imefanya mambo fulani ya maendeleo. Ni kama A atayarishe shamba (afyeke pori), alime na apande mbegu, B apalilie na kumwagilia, na kurudishia mbegu ambazo hazikuota, C atunze miche, afanye pruning na anyunyizie dawa ya kuua wadudu, D avune na kutunza kwenye ghala, E auze na kuweka fedha benki na D atumie hizo fedha kufanya maendeleo. Hapa utaona kwamba kila awamu ni muhimu. Ili ionekane kwamba viongozi wote hao wamefanya kazi nzuri tungetumia jina "serikali ya Tanzania" imefanya hivi. Kwa nini? Kwa sababu kuna mchango wa awamu zilizotangulia na kila awamu imejitahidi kwa kiasi chake. Awamu moja inaweza kufanya vizuri zaidi katika jambo X na awamu nyingine ikafanya vizuri zaidi katika jambo Y. Kwa mfano, awamu ya kwanza ilifanya vizuri zaidi katika afya na elimu - watoto wote (wa maskini na matajiri) waliweza kutibiwa na kusoma bure (kwa usawa).
 
Rais Samia, watanzania wote wakiwemo walioasisi wazo hilo wanastahili pongezi.
Haya mabishano ya nani ni nani katika miradi inayotumia kodi (jasho la watanzania wote) ni ujuha tu.
Kila mmoja amechangia kwenye nafasi yake.
Tunahitaji watu waondokane na utumwa wa fikra, wawe huru kwa mustakabali mwema wa taifa.
Haha kabisa aiseee,
Habari za kusema fulani kajenga as if katoa hela mfukon mwake ni ujuha
 
Haha kabisa aiseee,
Habari za kusema fulani kajenga as if katoa hela mfukon mwake ni ujuha
Tunatakiwa tuheshimu viongozi, wananchi wote, kwa nafasi zao.
Msingi wa usawa wa binadamu na Uhuru ujengwe kwenye fikra za watu wetu na vizazi vijavyo. Kubeza viongozi au raia wengine hakuna faida zaidi ya kujenga chuki.
Hata hivyo, matendo mabaya ya viongozi (kwa kuwa yanaathiri wote) lazima yakemewe na yawekwe kwenye record kwa mafunzo.
 
Back
Top Bottom