VIDEO: Hili lilimshinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete hata Magufuli. Rais Samia apongezwe

Aliienga kwa aslimia 15% na alonenga kwa asilimia,85% ni nani wa kumsifu?
Kunenga ndo nini mkuu?

Unahisi mama Samia alikuwa na choice kwa hali ilivyokuwa na status ya mradi ulivyokuwa umefikia?

But sijui hata tunabishana nini wakuu, kwani akijenga JPM na akijenga Samia what is the difference kwa watanzania? Hii ndio shida ya nchi kutokuwa na vipaumbele kama Taifa, kila kitu kinafanywa kwa matakwa ya Rais aliyepo madarakani matokeo yake mnaona kama anawafanyia favour

Ujinga mtupu.
 
Ifahamike pia kuwa hiyo movie ya Tarzan raia wameshaisahau kabisa
 
Lakini hebu tuwe wakweli mtu kachukua mradi ukiwa 35%,

Hivi unajua hii hata nusu ya Mradi ilikuwa bado?
Ishu hapa ni ujasiri wa kuasisi hiyo miradi.
Mama ameshaasisi nini cha maana so far?.
Kama chuma kingekuwa hai kingekuwa na hii miradi aliyoiacha tu mpaka leo? Kuuza rasilimali kwa kigezo cha uwekezaji ni kukusa ujasiri na ubunifu wa miradi mipya na kutoamini watu wako.
 
Mama ni kiongozi mzuri sana sema kila siku nasema shida iko kwa alio waamini wapige kazi ndo wanamwangusha sana tena sio kidogo.Wanakuja na stori za mama anaupiga mwingi kumsifia kinafiki uku wanamwangusha na kumpaka matope.Mama kama angepata watu kumi km makonda sidhani hata kama tungekua tunapiga kelele.
 
Samia mwamba sana hapa Duniani kwa hekima na akili nyingi
 
Sahihi hawa wengi wao si waaminifu
 
1. Umeme ni Magufuli
2. SGR ni Magufuli
3. Kuuza Bandari Samia
4. Kuuza KIA Samia
5. Kuuza Misitu Samia
6. Kuuza Ngorongoro Samia
7. Kuuza Ardhi ya Tanganyika Samia.

Mengine yote porojo.
Tuna dili na viumbe hai ...miaka 3 ya samia imeonyesha uwezo wake
 
Hapo umeongea kama mtanzania ..hawa kenge wengine wanaongea kama wao ni wana siasa
Mambo ya siasa tuwaachie wenyewe sie tufocus na maendeleo anayofanya na anapokesea tunapaza sauti na sio kuleta matuc kama sativa
 
Mimi ningeiweka hivi. Kila awamu imefanya mambo fulani ya maendeleo. Ni kama A atayarishe shamba (afyeke pori), alime na apande mbegu, B apalilie na kumwagilia, na kurudishia mbegu ambazo hazikuota, C atunze miche, afanye pruning na anyunyizie dawa ya kuua wadudu, D avune na kutunza kwenye ghala, E auze na kuweka fedha benki na D atumie hizo fedha kufanya maendeleo. Hapa utaona kwamba kila awamu ni muhimu. Ili ionekane kwamba viongozi wote hao wamefanya kazi nzuri tungetumia jina "serikali ya Tanzania" imefanya hivi. Kwa nini? Kwa sababu kuna mchango wa awamu zilizotangulia na kila awamu imejitahidi kwa kiasi chake. Awamu moja inaweza kufanya vizuri zaidi katika jambo X na awamu nyingine ikafanya vizuri zaidi katika jambo Y. Kwa mfano, awamu ya kwanza ilifanya vizuri zaidi katika afya na elimu - watoto wote (wa maskini na matajiri) waliweza kutibiwa na kusoma bure (kwa usawa).
 
Haha kabisa aiseee,
Habari za kusema fulani kajenga as if katoa hela mfukon mwake ni ujuha
 
Haha kabisa aiseee,
Habari za kusema fulani kajenga as if katoa hela mfukon mwake ni ujuha
Tunatakiwa tuheshimu viongozi, wananchi wote, kwa nafasi zao.
Msingi wa usawa wa binadamu na Uhuru ujengwe kwenye fikra za watu wetu na vizazi vijavyo. Kubeza viongozi au raia wengine hakuna faida zaidi ya kujenga chuki.
Hata hivyo, matendo mabaya ya viongozi (kwa kuwa yanaathiri wote) lazima yakemewe na yawekwe kwenye record kwa mafunzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…