Katika watu wenye biashara za ujanja ujanja basi ni huyu GSM na watu hii kampuni imemuweka Ghalib kama msimamizi tu lakini wenye hisa wamefichwa kwenye uvungu wa kitanda. Hii kampuni akiingia Rais asiyetaka mianya ya Rushwa basi GSM inaenda kutaifishwa iwe Mali ya umma maana biashara zote wanazofanya ni uwizi mtupu.
GSM ni muhuni sana alipoona swala la kiwanja walichouziana na Paul makonda tena mnamo mwaka 2013 makonda hajawa hata kiongozi wa serikalini, ametafuta wanasheria wenye njaa kuunda ushahidi wa michongo na kwa kuwa asilimia kubwa ya hii kampuni inakaliwa na former top government leaders kutoa amri wizara ya ardhi ifoji nyaraka ni kitu cha sekunde tu. Chuki ni mbaya Sana huyu makonda wanaomfanyia hizi hila ni wale waliosema ngoja afe tuone Nani atamtetea.
Uongozi wa Paul makonda ulikuwa ni wakiimra na kutojali misingi bora ya utumishi wa umma lakini Hili haliharalishi yeye kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi hata kama ni Mali yake kihalali na kafata taratibu zote za kisheria za Hati miliki. Kuna watu wanafrahi kuona huyu dogo analialia bila msaada lakini tujue kuwa nani yupo salama Kati yetu kama mifumo kandamizi bado ipo kila kukicha? Jibu nikuwa hakuna aliye safe maana ipo siku yatakukuta halafu utakuja mbele ya midia unafuka makamasi unaomba tupaze sauti.
HITIMISHO. Kampuni ya GSM sio ya waarabu, niyaviongozi matapeli wala rushwa na wenye ubinafsi na tamaa ya mali huyu mwalabu ni kivuli tu mwili umejificha. Makonda ameporwa kwa Chuki zao binafsi kipindi cha uongozi wa mwendazake.
View attachment 2147863View attachment 2147865