Mimi nadhani binadamu yeyote yule suala kama hilo linaweza kumtokea sehemu yoyote ile.
Hata walinzi wa Rais ni binadamu pia.
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1996. Kuna watu waliandaa sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Rais Nyerere.
Alikuwa anafikisha umri wa miaka 74. Sikumbuki ilifanyikia wapi….could have been at the Diamond Jubilee hall.
Sasa wakati Rais Nyerere anatoa Maneno ya shukurani, akasema kwamba hana shaka kuwa naye ataishi muda mrefu na kutimiza miaka 100, umri ambao mama yake mzazi aliufikia.
Akasema kwamba haoni sababu ya kwa nini hatofikia umri huo maana afya yake ni njema.
Akasema labda apondwe na gari/ basi ndo labda hatoufikia umri kama huo wa mama yake.
Fast forward three years later, what happened?
And compared to most Tanzanians or even most people around the world, he probably had access to the best healthcare.
Presidential bodyguards are human beings also. They get sick just like the rest of us do.
Yule mzee ukimsikiliza vizuri unaweza kuhoji imani yake kwa Mungu.
Kwa sababu typically watu wanaoamini Mungu wanamuachia Mungu suala la kifo, yeye alijiwekea sehemu kubwa sana ya kuweza ku control suala hilo.
Tatizo la kuangalia suala kama hili la mlinzi ni kwamba watu wengi wana hasira na serikali na wanatolea hasira zao kwenye issue kama hii bila ushahidi. Hence the unsupported claims of nepotism.
Sasa mtu anakimbilia kusema hii ni nepotism bila hata ushahidi, wakati hii inaweza kumtokea mtu yeyote, au hata kama kuna uzembe kwenye recruitment si lazima iwe nepotism.
Na unaweza kukuta huyo mlinzi ni victim wa kuwa overworked, na yeye anataka kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa bila kukataa kuwa overworked. Unaona hata hapo anataka kuanguka wenzake wanataka kumchukua akae chini, hataki. Anaona kama kukubali kukaa ni ku fail kufanya kazi yake ya kumlinda rais, wakati inawezekana kukaa chini kukawa tofauti ya yeye kuishi na kufa. Unamlinda vipi rsis wakati hata wewe mwenyewe huwezi kusimama?
Ila, ukisoma kitabu cha mlinzi wa zamani wa Nyerere Peter D.M Bwimbo "Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere" ukaona wanavyofundishwa loyalty utaelewa kwa nini hakutaka kukaa.
Sasa wabongo wengi wanaweza kuja hapa kumshambulia victim bila kujua kiini.
Kwa kuichukia serikali tu.