Video: Nape alipoangua kilio hadharani jimboni kwake Mtama

JPM kuendelea kumkumbatia Bashite ndo anachukiza sana wananchi. Mdharau mwiba guu huota tende. Alidharau ishu ya bashite kufoji vyeti kadiri muda unavyozidi kwenda yanazidi kuibuka mambo mengi in relation to Bashite.
 
.... Si nyie majuzi mlishikwa na mizuka kwamba Halima Mdee kutukana mjengoni? Angalia mnavyomwaga mitusi hapa...

mkuu umenifananisha!! acheni ujinga wa kumuweka mtu upande fulani kisa anawaza tofauti na wewe!! acha

utakuja kumuweka mama yako upande wa wanaume kwa sababu tu kafanya jambo fulani
 
nape ; umekosea; umeshavuka mstari; haupo na sisi tena
 
Nape ashaona uchaguzi wa 2020 utakua mgumu sana kwa CCM ameona bora aanze kujisafishia njia jimboni mwake mapema
 
MTU mzima kulialia hadharani ni dalili za uoga
 
hata haya huna mtoto wakike..mishipa umetoa lkn unaongea utumbo ili uonekane umecomment. .ovyo kbsa

Kama wewe upo ovyo haswaaa, basi sio unipangie mimi niposti wapi. Ishi maisha yako, mtanyooka tu.
 
Umejibu vizuri kudos
 
Mbona kwenye mkutano wake hawapigi nyimbo za chama tawala
 
Wewe ni bure tu! Kwani Tanzania ni Jimbo la Nape? Ubunge wenyewe alipewa kwa mbinu chafu, kweli kesho akiachiwa ataupata?
Nape ana nini zaidi ya bingwa Lowasa? Mbona Lowasa ametulia? Au vipi wakati Zitto anajifaragua kuomndoka CDM, yuko wapi leo hii? Ni mbunge asiye na jukwaa na wenzake wanaanza kuondoka na kupata nafasi serikalini.
 
Mimi huwa sibabaishwi na machozi ya wanasiasa. Ndo zao wanapotaka kupata huruma ya wananchi. Alianza baba yake Pinda naona na yeye kaiga. Hata Obama rais wa taifa lenye nguvu nae analia. Ni unafiki wa hali ya juu ndo maana majuu wanaita [HASHTAG]#WaterWorks[/HASHTAG]

Kama yeye analia kwa sapoti anayopata kwa wananchi wake, mimi nalia kwa kiongozi kama yeye kukubali kutembea juu ya migongo ya kina mama. Nape kwa kile kitambi chake sio wa kutembea hata kwenye tumbo la mtu, achilia mbali mgongo ambako kuna kiungo muhimu na rahisi kuharibiwa-yaani uti wa mgongo. Ni hatari kiafya kutembea juu ya mwili wa mtu. Tulimfukuza mkoloni kwa sababu ya kuamini binadam wote ni sawa na wanapaswa kuheshimiwa. Kukubali kutembea juu ya mwili wa mtu ni kutukumbusha umwinyi na utumwa ambao uliwatesa babu zetu. Iwe mwisho kwa mwanasiasa kubebwa kama maiti au kutembea juu ya miili ya wake za watu. Ni udhalilishaji usio kifani, bila kujali kama wamejitolea wao wenyewe. Mtu akijitolea umuue na wewe ukamuua huwezi kukwepa lawama.
 


Wachaga wenzako wanaparurana huko akina Ndesamburo wewe umekalia CCM, achana na CCM ni Chama kubwa na inaongoza Dola shughulikia mgogoro wa Wachaga wenzako huko chadema mpate Mwenyekiti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…