Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

...Watanzania Wengi ni Wastaarabu. Tunapisha Ambulance, Zimamoto na Polisi zikiwa na Dharura.
Magari yote hukaa Kando ili kupisha Wapite. Tulianzia Tena kuwatafutia njia Kushoropa, tuvunja Sheria Zetu Wenyewe..Barabara ya Mwendokasi Ibaki ya Mwendokasi!!
 
Soma sheria za matumizi ya hizo barabara. Acheni mazoea. Mkiona kifoleni kidogo tu mnarukia njia ya mwendokasi au wrong way.
Gari za zimamoto na ambulance zinaruhusiwa kupita wakati wa dharula nyingi mliozoea kipindi sheria mpaka kibali.
Na mimi nimezungumzia wakati wa dhararu kwa magari ya dharura tu i.e. ambulance, polisi na zimamoto. Magari ya binafsi marufuku hata awe mkuu wa Mkoa. Na polisi pia wanapokuwa kwenye safari za kawaida marufuku. Raia ndiyo kabisa hawaruhusiwi. Kama Tanzania wameweka sheria kuwa magari ya zimamoto, polisi na ambulance hayaruhusiwi kupita wakati wa dharura basi ni makosa makubwa. Inakujia kwenye akili kwamba Manzese kuna nyumba inayoungua na zimamoto wako Magomeni lakini wameshindwa kwenda kwa haraka kwa sababu kuna foleni na barabara ya mwendokasi hawapaswi kupita?
 
Kabisa. Awe askari, awe mkuu wa majeshi, awe mkuu wa mkoa, haruhusiwi kupita. Wanaoruhusiwa kupita ni polisi, zimamoto na ambulance wakati wa dharura tu. Hawa polisi kama walikuwa wanakwenda kwenye lindo basi ni makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…