Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

Hii barabara inatumika pia kama emergency, chukulia ndugu yako amepandishwa kwenye ambulance na mnawahi labda Muhimbili mnazuiwa hivyo na anatumia oxgen au pili nyumba yako inaungua moto halafu zima moto wanazuiwa hivyo au hata pia wamepewa taarifa kuna mahali kuna panya road wanakuja halafu mnawazuia halafu kesho yake aliyejeruhiwa ni ndugu yako.

sio sawa.
...Watanzania Wengi ni Wastaarabu. Tunapisha Ambulance, Zimamoto na Polisi zikiwa na Dharura.
Magari yote hukaa Kando ili kupisha Wapite. Tulianzia Tena kuwatafutia njia Kushoropa, tuvunja Sheria Zetu Wenyewe..Barabara ya Mwendokasi Ibaki ya Mwendokasi!!
 
Soma sheria za matumizi ya hizo barabara. Acheni mazoea. Mkiona kifoleni kidogo tu mnarukia njia ya mwendokasi au wrong way.
Gari za zimamoto na ambulance zinaruhusiwa kupita wakati wa dharula nyingi mliozoea kipindi sheria mpaka kibali.
Na mimi nimezungumzia wakati wa dhararu kwa magari ya dharura tu i.e. ambulance, polisi na zimamoto. Magari ya binafsi marufuku hata awe mkuu wa Mkoa. Na polisi pia wanapokuwa kwenye safari za kawaida marufuku. Raia ndiyo kabisa hawaruhusiwi. Kama Tanzania wameweka sheria kuwa magari ya zimamoto, polisi na ambulance hayaruhusiwi kupita wakati wa dharura basi ni makosa makubwa. Inakujia kwenye akili kwamba Manzese kuna nyumba inayoungua na zimamoto wako Magomeni lakini wameshindwa kwenda kwa haraka kwa sababu kuna foleni na barabara ya mwendokasi hawapaswi kupita?
 
Stupidity at its best!
Hii nchi huwa tunawaza kwa kutumia nini? Yani unakaa kabisa na akili timamu unashauri watu wawe wanaruhisiwa kukatiza na magari kwa sababu tu ni kada fulani?


Wakuu iko hivi: inapokua dharura kama ni zimamoto au gari la wagonjwa au dharura ya kiusalama inaeleweka na hakuna ambaye hapendi askari wapite .

Ila hili la kusema flani apite ni la hovyo vipi mmewaza daktari aliyeitwa kwenye emergence naye angepita hapo?

Tuacheni vituko!
Kabisa. Awe askari, awe mkuu wa majeshi, awe mkuu wa mkoa, haruhusiwi kupita. Wanaoruhusiwa kupita ni polisi, zimamoto na ambulance wakati wa dharura tu. Hawa polisi kama walikuwa wanakwenda kwenye lindo basi ni makosa.
 
Back
Top Bottom