Mkuu 'Zawadi', hili la majina ni swala dogo sana kwangu, na hapo niliandika "Tanzania Bara" kwa bahati mbaya tu kwa kuwa naandika haraka sana. Kwa hiyo tusipoteze muda kwenye maswala yasiyokuwa na maana yoyote. Tujikite kwenye maswala mazito kama huo muungano ulikuwa muungano wa nini hasa; kama lengo lilikuwa baadae sehemu moja ya muungano huo ianze kwa upande wake kujitambulisha kuwa wao ni nchi, tena bila kujali yule waliye ungana naye?Sikiliza vizuri! Katika mkataba ni nchi mbili ndio ziliungana. Tanganyika na Zanzibar na mipaka yake iko wazi kabisa. Katika mkataba ule jina Tanzania bara halipo. Ok, umeamua kuita Tanzania bara, sawa, hivi mipaka yake ni ipi? Nafikiri tutakubaliana kuwa ndio ile ile ya Tanganyika. Hapa nakusihi mwenzangu na watanzania wote msidanganyike na kuwapa CCM uhalali wa kile ambacho hukihalalishi.
Sasa Zanzibar ni nchi; lakini hata yenyewe imeungana na nani na muungano huo una umuhimu upi kwao, iwapo wanajiendeshea mambo yao kama nchi.
Sasa taratibu zitafanyikia wapi, kama serikali na Bunge hawawezi kujadili na kuweka taratibu za muungano huo?Muungano hauamuliwi Bungeni wala serikalini, na ukifanya hivyo umeulazimisha muungano
Hili swala la "kulazimisha" umelirudiarudia sana humu, kiasi kwamba sasa naanza kuona ubatili wa hoja hiyo. Hakuna anayemlazimisha yeyote kuwa kwenye muungano. Sijui hii dhana inatoka wapi, na nidhana potofu kabisa inyotumiwa visivyo. Tanganyika hawajamlazimisha yeyote kubaki ndani ya muungano. Baraza la wawakilishi Zanzibar wamepitisha mambo mengi sana yanayoihusu Zanzibar, bila hata kushirikishwa kwa njia yoyote kwa mshiriki wake ktk muungano Tanganyika, wala Bunge la Tanzania, ambako kuna wawakilishi toka Zanzibar. Sasa hapa unaniambia wawakilishi hawa hawawezi kulizungumzia swala la Zanzibar kujiondoa moja kwa moja ndani ya muungano. Kwa nini? Wanaogopa kupoteza maslahi Zanzibar inayoyapata toka kwa haya mazezeta ya Tanganyika?
Wawakilishi katika Baraza lao wanatunga sheria zote za Zanzibar. Wamepitisha Katiba yao, wamepitisha bendera ya nchi yao, wameainishi mipaka ya nchi yao, na kurasimisha mali zote zilizomo ndani ya mipaka hiyo kuwa yake; halafu sasa watu wanageuka na kusema Zanzibar wanalazimishwa kuwa ndani ya muungano!
Unapokula na kipofu ni lazima uwe mwangalifu sana. Zanzibar sasa imegusa mkono wa huyu kipofu.
Mwisho: tusisahau kwamba huko huko Zanzibar kuna watu wanaoupenda huu muungano si kwa sababu za kichoyo kama ilivyo kwa baadhi yao, na pia kuna kundi ambalo siku zote limekuwa likichochea muungano kuvunjika. Ni kundi hili ndilo linalohusika na ubunifu wa KERO chungu nzima zisizo na kikomo. Hili kundi limeruhusiwa kushika hatamu na linafanikiwa sana.
Hii dhana ya "Muungano wa Kulazimishwa" inatoka huko huko; lakini nasema hivi, kuna mawili> Moja Tanganyika ichukue jukumu la kuuvunja muungano moja kwa moja bila ya simile; au Tanganyika iweke mguu chini na kulinda muungano kwa njia yoyote ile. Inawezekana sana.