Video: Tundu Lissu atoa ufafanuzi wa hoja aliyoitoa Babati Aprili 26, 2024 kumjibu Fatma Karume kuhusu 'Ubaguzi na Muungano wetu'

Mkuu 'Zawadi', hili la majina ni swala dogo sana kwangu, na hapo niliandika "Tanzania Bara" kwa bahati mbaya tu kwa kuwa naandika haraka sana. Kwa hiyo tusipoteze muda kwenye maswala yasiyokuwa na maana yoyote. Tujikite kwenye maswala mazito kama huo muungano ulikuwa muungano wa nini hasa; kama lengo lilikuwa baadae sehemu moja ya muungano huo ianze kwa upande wake kujitambulisha kuwa wao ni nchi, tena bila kujali yule waliye ungana naye?
Sasa Zanzibar ni nchi; lakini hata yenyewe imeungana na nani na muungano huo una umuhimu upi kwao, iwapo wanajiendeshea mambo yao kama nchi.
Muungano hauamuliwi Bungeni wala serikalini, na ukifanya hivyo umeulazimisha muungano
Sasa taratibu zitafanyikia wapi, kama serikali na Bunge hawawezi kujadili na kuweka taratibu za muungano huo?
Hili swala la "kulazimisha" umelirudiarudia sana humu, kiasi kwamba sasa naanza kuona ubatili wa hoja hiyo. Hakuna anayemlazimisha yeyote kuwa kwenye muungano. Sijui hii dhana inatoka wapi, na nidhana potofu kabisa inyotumiwa visivyo. Tanganyika hawajamlazimisha yeyote kubaki ndani ya muungano. Baraza la wawakilishi Zanzibar wamepitisha mambo mengi sana yanayoihusu Zanzibar, bila hata kushirikishwa kwa njia yoyote kwa mshiriki wake ktk muungano Tanganyika, wala Bunge la Tanzania, ambako kuna wawakilishi toka Zanzibar. Sasa hapa unaniambia wawakilishi hawa hawawezi kulizungumzia swala la Zanzibar kujiondoa moja kwa moja ndani ya muungano. Kwa nini? Wanaogopa kupoteza maslahi Zanzibar inayoyapata toka kwa haya mazezeta ya Tanganyika?

Wawakilishi katika Baraza lao wanatunga sheria zote za Zanzibar. Wamepitisha Katiba yao, wamepitisha bendera ya nchi yao, wameainishi mipaka ya nchi yao, na kurasimisha mali zote zilizomo ndani ya mipaka hiyo kuwa yake; halafu sasa watu wanageuka na kusema Zanzibar wanalazimishwa kuwa ndani ya muungano!

Unapokula na kipofu ni lazima uwe mwangalifu sana. Zanzibar sasa imegusa mkono wa huyu kipofu.

Mwisho: tusisahau kwamba huko huko Zanzibar kuna watu wanaoupenda huu muungano si kwa sababu za kichoyo kama ilivyo kwa baadhi yao, na pia kuna kundi ambalo siku zote limekuwa likichochea muungano kuvunjika. Ni kundi hili ndilo linalohusika na ubunifu wa KERO chungu nzima zisizo na kikomo. Hili kundi limeruhusiwa kushika hatamu na linafanikiwa sana.
Hii dhana ya "Muungano wa Kulazimishwa" inatoka huko huko; lakini nasema hivi, kuna mawili> Moja Tanganyika ichukue jukumu la kuuvunja muungano moja kwa moja bila ya simile; au Tanganyika iweke mguu chini na kulinda muungano kwa njia yoyote ile. Inawezekana sana.
 
Hakuna kinachofanyika bila ushiriki wa Bunge sehemu yoyote ile. Zanzibar haikuungana peke yake; na wala haikuilazimisha Tanganyika waungane. Kulikuwepo na majadiliano kati yao na wakakubaliana waungane.
Kwa hiyo, hata hiyo referendum unayosema, ni lazima swala hilo liingizwe Bungeni, hakuna njia nyingine yoyote ya kulianzisha.
Na kwa bahati mbaya sana, hata huko Zanzibar, pamoja na kuwa na Baraza la Wawakilishi, serikali ya Zanzibar haina uwezo wa kuitisha kura ya maoni ya waZanzibari kuhusu muungano. Kwa hiyo Tanganyika haiepukiki kwa njia yoyote.
 
nilimsikia Mbowe anasema zanzibar imeleta wabunge 80 kwenye bunge la jamhuri, kwa kipi zaidi? Tanganyika tulipigwa woga na watu wanaogopa kujadili muungano wakati wazanzibar wanaruhusiwa kuujadili na wanazidi kuneemeka.
 
Kwa nilivyomsikiliza Lissu, nihitimishe kusema, sisi wabara tunamatatizo ya kiafya ya akili
Hilo halina shaka...

Mtu kutoka nchi nyingine iitwayo Zanzibar yenye population watu wasiyozidi 1,800,000 anaweza vipi kuja kuwa Rais ktk nchi nyingine iitwayo Tanganyika yenye population ya watu zaidi ya 64,000,000...???

Hii inaingia akilini kweli? Muungano gani huu wa kijinga hivi aisee...?

Nchi na taifa la Zanzibar lipo mpaka leo, wana serikali yao na wana mfumo wao wa kujitawala...

Sisi Tanganyika yetu iko wapi? Ilipotolea wapi? Serikali na mfumo mzima wa kujitawala sisi wenyewe uko wapi..??

Watanganyika tuna akili kweli? Aisee ni nani huyo aliyetuloga tukawa hatuna akili kiasi hiki..??
 
Mtu kutoka nchi nyingine iitwayo Zanzibar yenye population watu wasiyozidi 1,800,000 anaweza vipi kuja kuwa Rais ktk nchi nyingine iitwayo Tanganyika yenye population ya watu zaidi ya 64,000,000...???
Mtu kutoka nchi yenye watu 64,000,000 yeye anayo haki ya kuitawala nchi yenye watu 1,800,000? Hii hija haina mashiko, kwani ni mazungumzo/porojo za uongo.

Mtu huyu kutoka Zanzibar ana haki sawa ya kutawala na kuongozwa na mtu yeyote - awe katoka Tanganyika/Bara au Zanzibar.

Akili za kikoloni hizi za kutoka Afrika. Kama kawaida Mwafrika unajifananisha na asiyekuwa Mwafrika kwa uovu.
Hii inaingia akilini kweli? Muungano gani huu wa kijinga hivi aisee...?
Mkuu hii inaingia akilini kwa wenye akili na utu.

Mkuu huu ni muungano wa Kiafrika, ulioasisiwa Afrika. Ni muungano wa kipekee; haupatikani popote duniani.
 
Tatizo kubwa ni viongozi wa kutoka Tanganyika wala siyo Zanzibar.
 
kuhusu bandari na Ngongoro anaongea upuuzi ila muundo wa muungano haufai.
 
kuhusu bandari na Ngongoro anaongea upuuzi ila muundo wa muungano haufai.
Ungejitahidi ingalao kidogo kuonesha huo upuuzi wake kuhusu Bi Samia Suluhu Hassan (Mzanzibari) kuuza bandari, mamilioni ya misitu na mbuga zetu za wanyama (Ngorongoro, Loliondo na za chinihchini na Serengeti inanyemelewa) kwa hao hao majomba na babu zake waarabu wa Oman na Dubai...

Onesha upuuzi wake uko wapi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…