DOKEZO VIDEO: Wazazi angalieni Walimu Shule ya Sekondari Majaliwa

DOKEZO VIDEO: Wazazi angalieni Walimu Shule ya Sekondari Majaliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwaiyo mbadala wa kutoa usumbufu kwa watoto ndo kuwapiga kama wanaua nyoka? Waalimu wanatengeneza kizazi cha watu makatili….nimesoma shule ya kata tulikua tunapigwa mpaka wanafunzi wengine waliacha shule kwasababu ya kupigwa kama hivo [emoji174]

Na kuhusu swala la uwezo wa kuyamudu masomo sometimes ni juhudi za mwalimu husika wa somo na siku hizi walimu mwenyewe hawana huo ueledi wanaitisha tu hela za tuition usipolipia ndo imekula kwako.
Hii ni mbaya sana. Ukatili kwa watoto na wanafunzi una athari mbaya sana na za muda mrefu.

HAIFAI, HAIFAI, HAIFAI, HAIFAII!!!!!!!!

Kwanza, kwani ni lazima kila mtu asome au afaulu?

Wasioweza kuendana na shule waondolewe na sio kuumizwa!
 
Wapumbavu mnapata mda wa kurecord kwann msimzue huyo Jamaa au kuongea naye asichape Sana watu wapumbavu Kama mtoa post , aliyelocord mnabidi kukamatwa na kuingizwa ndani magereza huku mitandaoni tumewachoka.
 
Kwaiyo mbadala wa kutoa usumbufu kwa watoto ndo kuwapiga kama wanaua nyoka? Waalimu wanatengeneza kizazi cha watu makatili….nimesoma shule ya kata tulikua tunapigwa mpaka wanafunzi wengine waliacha shule kwasababu ya kupigwa kama hivo [emoji174]

Na kuhusu swala la uwezo wa kuyamudu masomo sometimes ni juhudi za mwalimu husika wa somo na siku hizi walimu mwenyewe hawana huo ueledi wanaitisha tu hela za tuition usipolipia ndo imekula kwako.
Mimi siungi mkono adhabu kali kupitiliza kwa watoto. Huo ni ukatili. Ila ni ukweli kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000 zilipoanzishwa shule za kata, kumekuwepo na ongezeko kubwa la watoto wanaoingia sekondari. Na hapo ndipo tatizo lilipoanzia.

Maana kumekuwepo na utaratibu wa kuchukua wanafunzi darasa zima kutoka shule za msingi, na wote kwenda sekondari. Watoto wamegawanyika katika makundi matatu. Wenye uwezo mkubwa wa kuelewa kwa haraka (fast learners), na wale wenye uwezo mdogo wa kuelewa mambo jwa haraka (slow learners).

Kundi la watoto wenye uwezo mdogo, linamudu elimu ya kutumia matendo zaidi kuliko akili nyingi. Mfano elimu ya ufundi, stadi za kazi, nk. Na mtoto wa aina hiyo hata umfundishe vipi, uwezekano wa kufeli ni mkubwa kuliko kufaulu. Na hawa ndiyo mara zote huingia kwenye mitafaruku na walimu wenye msongo wa mawazo.

Ni jambo jema serikali imeliona hili tatizo. Huenda mtaala mpya ukianza kutumika, utakuwa ni mwarobaini wa hayo matatizo yote.
 
Wapumbavu mnapata mda wa kurecord kwann msimzue huyo Jamaa au kuongea naye asichape Sana watu wapumbavu Kama mtoa post , aliyelocord mnabidi kukamatwa na kuingizwa ndani magereza huku mitandaoni tumewachoka.
Unajuaje utata wa huyo mwalimu Kwa wenzake
 
Very light punishment kama hizo watu wanaanzisha mjadala... Hii si sawa kabisa.
 
Mtu unamuona anamchapa mtoto sana au anapitiliza ! Kwanini huo muda wa kumrekodi usitumie kumnyang'anya fimbo huyo mwalimu?

Ili asimuumize mtoto !! Serikali iwe inawafukuza hata wanaorekodi ! Jifunzeni kuonyana na kuelemishana nyie kwa nyie.

Yaani kama una uwezo wa kushuhudia na kurekodi mtoto anapigwa hivyo , maana yake hata wewe ni katili unamrekodi katili mwenzio.

Huku mtandaoni tumewachoka ! Kila siku nyie kurekodiana tu au ndo fashion Walimu
Ni upumbavu mkubwaa...
 
Tuna haki ya kusema kada ya walimu imeingiliwa na watu wasiojielewa
Very true .. kumejaa wapumbavu... Nafikiri ni hawa wanaojitolea.... Wachache...nafahamu wapo wastaarabu
 
Huu upuuzi utaisha lini lakini....

Why this!?? Kwanini tunarekodi... Kwanini tusheee....
Lazima turekodi ili uhuni uanikwe.

Huyu mwalimu akamatwe afunguliwe mashtaka ya KIMAADILI na ya JINAI pia.

MASHTAKA YA KIMAADILI - Kuwa mkaidi kufuata miongozo ya Wizara ya elimu na ya kisheria.

MASHTAKA YA JINAI - kufanya shambulio la mwili na kudhuru.
 
Ni jambo jema serikali imeliona hili tatizo. Huenda mtaala mpya ukianza kutumika, utakuwa ni mwarobaini wa hayo matatizo yote
Huo mtaala mpya hautokuja kuuona na hata mabadiliko ya maana hautayaona toka mwaka 2000 mpk leo pamefanyika marekebisho mangapi ?na upi ufanisi wa hayo maboresho,, udhaifu wa elimu yetu ndio mtaji wa wanasiasa...na hakuna mwanasiasa anaetaka mageuzi ya kumpindua mwenyewe ...Ni Kama vile ccm isivyotaka KATIBA MPYA kwasababu inajua kitachoikumba
 
Lazima turekodi ili uhuni uanikwe.

Huyu mwalimu akamatwe afunguliwe mashtaka ya KIMAADILI na ya JINAI pia.

MASHTAKA YA KIMAADILI - Kuwa mkaidi kufuata miongozo ya Wizara ya elimu na ya kisheria.

MASHTAKA YA JINAI - kufanya shambulio la mwili na kudhuru.
Wewe ni poyoyo mmoja...
 
Juzi niliwakamata watoto wakivuta bangi na kucheza kamari..... Wakanipa buku 2 kila mmoja mara 6 nikapitia kwa mangi kuchukua mchele kilo 2 na nyama nusu na robo
Safi sana Nkuu, maana matoto yenyewe baba na mama zao ndio Hawa wanaolialia hapa, kwa nini ujisumbue
Waache wavute bangi wakawapiga ngwara baba zao na kuwakaba mama zao
 
Very light punishment kama hizo watu wanaanzisha mjadala... Hii si sawa kabisa.
Very light punishment!!?

Hebu tega makalio nikupige fimbo ishirini za moto kama hujanya wewe!!

Okey, kwa sababu inaonesha dhahiri ninyi ni wakaidi, basi wacha muendelee kushughulikiwa tu. Hatua zinapochukuliwa msihamaki.

UMESHAELEZWA, viboko vinatolewa kwa utaratibu. Tena kwa idhini ya kimaandishi kutoka kwa MKUU WA SHULE na visizidi vinne!!

Ukikiuka au kujeruhi mwanafunzi utashughulikiwa! Hiyo ni hakika.

Na mimi nasema waendelee kuwarekodi na kuwachukulia hatua!

Kazi ikiwashinda mkafuge kuku.
 
Back
Top Bottom