Moja kwa moja.
Kwanza kabisa niweke wazi kuwa Mimi sio Pro_Hamas wala Pro_Jews msimamo wangu kuhusu hii vita na yanayoendelea nimeelezea katika nyuzi hizi
Moja kwa moja.. 1. Kwa nini nawalaumu Hamas ? Sikatai ukweli kwamba Raia wa Palestine wameishi kwa mateso miaka mingi chini ya utawala wa Wazayuni,wakiuwawa kunyimwa haki za msingi nk na nakubali kwamba wanayo haki ya kupambana katika kujikomboa na madhila wanayopitia. Ninapowapinga ni njia...
www.jamiiforums.com
Mwingine
Moja kwa moja... Kabla sijaanza mada yangu ningependa kuweka wazi msimamo wangu wa tokea awali katika yale yanayoendelea Gaza ; 1. Siwaungi mkono Hamas na njia wanazotumia ambazo hazikubaki kidini wala kikawaida tu , ukijumlisha utekaji wao wa watoto , Wazee , wanawake na makandokando yao...
www.jamiiforums.com
Twende kwenye Mada...
Siku za Karibuni kulikuwa na taarifa kuwa watu 15 wa kutoa Msaada wa kibinadamu ya kitabibu huko Gaza wameuwawa wakiwa ndani ya gari ya kubebea wagonjwa "Ambulance " .
Hapo awali, Israel ilidai kuwa wanajeshi walifyatua risasi kwa sababu msafara ulikaribia "kwa mashaka" gizani bila taa za mbele au taa zinazowaka. Harakati za magari hayo hazikuwa zimeratibiwa au kukubaliwa hapo awali na jeshi.
Video ya simu ya mkononi, iliyorekodiwa na mmoja wa wahudumu wa afya waliouawa, ilionyesha magari yalikuwa na taa zimewashwa walipokuwa wakijibu wito wa kusaidia watu waliojeruhiwa.
Baada ya hapo miili yote waliikusanya kwa pamoja na kuifukia , mpaka baada ya wiki moja ilipogunduliwa na kipande cha video kukutwa ndani ya simu ya mmoja ya waliowawa .
Utata unaojitokeza
Official statement ya version ya story ya mauaji ya msafara kutoka mamlaka ya Israel kabla ya video , inapingana kabisa na yale yalionekana kwenye video hiyo na kuonyesha jinsi gani walivyokuwa waongo na mahodari wa kutunga uongo kuusambaza na kuupamba uonekane kuwa ukweli .
Sasa hili limeoneka wazi hapo isingekuwa ushahidi mpaka Leo watu wangeaminishwa uongo je , vipi katika mengine ambayo tunaendelea kuaminishwa na IDF kuhusu maaji ya raia na mgogoro huu kwa ujumla tuwaamini ?
Inasikitisha sana, baada ya kuumbuliwa wameamua kukiri uongo, wao kwani kuwa mkweli mtu unapungukiwa kuliko kutaka kuwaBrainwash machawa na wengineo ?
View attachment 3294599
#Uzi unaendelea