Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Nimekusoma. Kifurushi cha 25,000 kinatosha kabisa kwa mtu mmoja au wawili.

Hawa ni Konnect, wana kifurushi cha 20Mbit/s unlimited kwa mwezi kwa 60,000. Ila 60,000 kwa raia wa kawaida mambo mengi. Tunarudi palepale, 25,000.



 
Nipo mkuu sijaingia mitihi vifurishi vya Voda mfumo bado haiko vizur tgo vipo Kama kawaida

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Angekuwa ni mmingine angesema leteni hizo pesa hapa akazidakuna, ila wewe unaonekana ni muaminifu sana, ila hii hela niliyo iweka kwa m pesa ili hivyo vifurushi vikikaa poa nikutumia sinitaidakuna sasa mkuu? Fanyeni basi mpango mkuu kabla sijaidakuna hii hela.
 
Hii satellite internet speed yake ikoje Kwa ambae ameshatumia?! Mfano hcho kifurushi cha 20mbps Kwa matumizi ya nyumbani
 
Hii satellite internet speed yake ikoje Kwa ambae ameshatumia?! Mfano hcho kifurushi cha 20mbps Kwa matumizi ya nyumbani
Satelite internet weakness yake kubwa ni kwamba ina ping kubwa. Reviews za Konnect ping ni zaidi ya sekunde, assume unatype jamiiforums.com itasubiria kama sekunde kadhaa ndio itafunguka, hii inamaanisha vitu vyote vya live kama kuangalia mpira ama live video yoyote, video call, kupiga simu kama za whatsapp na kubrowse itakuwa slow vibaya mno.

Ila satelite yao jamaa nimeona ni 75GBps, ina speed vibaya mno, hivyo kama una matumizi ya kudownload ama kuangalia buffered video kama Netflix na youtube si mbaya.
 
Duh ushanipa wasiwasi wa kuitumia. Vipi hiyo Fiber ya TTCL chief coverage na speed yake ikoje
 
Fiber sijaitumia mkuu, ila adsl coverage ni kubwa sana Even mikoani ipo,
Kuna tofauti gani Kati ya Fiber na ADSL Mkuu?! Na Je vifurushi vya ADSL speed yake ikoje mfano Kwa range ya kifurushi cha 50k-60k?! Vinafaa Kwa matumizi ya nyumbani?!
 
Kuna tofauti gani Kati ya Fiber na ADSL Mkuu?! Na Je vifurushi vya ADSL speed yake ikoje mfano Kwa range ya kifurushi cha 50k-60k?! Vinafaa Kwa matumizi ya nyumbani?!
Adsl pia ni ya kizamani mkuu ila ina unafuu compare na Satelite.

Unakumbuka zamani enzi za modem za 3.2mbps? Kipindi cha 3g unasubiria movie nusu saa idownload. Expect speed kama hii kwa adsl.

Yenyewe inatumia zile waya za shaba ambazo zamani tulitumia kwenye simu za mezani. Na ukiunga adsl unapewa na namba yako kabisa inayoanziwa na 0222 kama ya simu za mezani.

Fiber ni mziki mwengine ipo fast sana hasa ping, ni 1ms ama 2ms, sometime wakati unabrowse ni kama hutumii internet ukigusa tu inafunguka. Sema coverage yake kwa sasa ni ndogo sana ipo tu mjini katikati.

Hivyo mkuu nenda tawi la TTCL karibu na Nyumbani ulizia, kama Fiber ipo kwako unga hio 20mbps kwa 55,000 ni bei nzuri sana.

Kama haipo covered adsl ndio option iliobakia. Adsl naona kifurushi cha 25000 na 50000 vina value zaidi 4mbps na 8mbps. Mimi siamini kama adsl ya TTCL inaweza gonga 8mbps hivyo nimechukua cha 4mbps, unaweza jaribu cha 50000 ukaleta feedback.
 
Shukrani sana Mkuu nimekupata.

Na vipi kufunga hizo adsl hamna gharama nyingine za installation zaidi ya hyo 25,000?!
 
Shukrani sana Mkuu nimekupata.

Na vipi kufunga hizo adsl hamna gharama nyingine za installation zaidi ya hyo 25,000?!
Inabidi ununue router yako mkuu. Kikawaida TTCL walikuwa wanatoza 55,000 kwa ajili ya vifaa ila wamemaliza kwa sasa. Router za Adsl ni ngumu sana kupata.
 
Kama kuna mtu ana access na Zuku fiber ajaribu. Kwa sasa sidhani kama kuna fiber ina kasi kama hiyo ile ngoma ina piga mpaka 100mbps. coverage yao ipo posta nadhani kwa sasa wata kuwa wame sogea mtaani zaidi. Ila kitu kama movie ya 1GB unatumia kama 10minutes ur done. Nipo mbali kidogo nayo kwa sasa ningeweka ila nita leta screenshot ya net test hapa.
Nimepata screen shot ya sasahivi. Ni saa tano sasahivi busy hour ikifika mida ya saa kumi kuendelea wakati watu wametoka maofisini ni 100mbps

 

Attachments

  • VID-20220127-WA0017.mp4
    879.9 KB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…