Vigezo na sifa za Mwanamke wa kuoa kwa 2024 - 2050

Vigezo na sifa za Mwanamke wa kuoa kwa 2024 - 2050

VIGEZO NA SIFA ZA MWANAMKE WA KUOA KWA 2024 - 2050

Anàandika, Robert Heriel.
Mtibeli

Pasipo kupoteza muda. Ikiwa wewe ni mwanaume unatafuta mke wa kuoa ili ujenge naye familia basi vigezo na sifa zifuatazo sharti Mwanamke huyo utakayemuita mkeo lazima awe nazo. Ili uishi maisha ya furaha.

Wanaume nitawagawa katika makundi matatu kulingana na umri kama ifuatavyo;
1. Wanaume wenye Miaka 20 - 35
2. Wanaume Wenye miaka 36 - 50
3. Wanaume wenye miaka 51 -. 85

1. Wanaume wenye Miaka 20-35
Ikiwa upo katika age hiyo na unatafuta Mke wa kuoa basi vigezo na sifa zifuatazo ni lazima, nasisitiza ni lazima uzingatie VIGEZO hivi ili ndoa na maisha ya familia yako yawe na furaha.
Vigezo na sifa hizo ni kama ifuatavyo;

Piga ua garàgaza, ukiwa na miaka kati ya miaka 20 - 35 na unatafuta kuoa basi hakikisha unaoa Mwanamke Bikra.
Elewa kama ilivyo ngumu kupata Mwanamke Bikra ndivyo hivyohivyo ni ngumu kuishi kwa furaha na Mwanamke asiye Bikra.
Elewa kuwa karne hii uzinzi na uasherati upo kwa kiwango cha juu kabisa.
Matumizi ya P2, utoaji wa mimba kwa kiwango cha kutisha, matumizi ya madawa na teknolojia ya kuzuia mimba yanaathari kubwa katika familia utakayoianzisha.
Sijazungumzia mambo ya kihisia kuhusu umuhimu wa bikra kwani Jokajeusi alivyokwisha kueleza.

Ni ngumu ukioa Mwanamke Bikra akasumbua kwenye mambo ya ujauzito, sijui homoni imbalance,
Elewa kuwa ukioa mke Bikra hakuna msamiati Ex kwani wewe ndio namba moja. Na wewe ndio utakuwa Ex wake wa kwanza ikiwa mtaachana.

Elewa kuwa ukioa Mwanamke Bikra hana makovu ya kihisia ya kutendwa hivyo wewe ndiye utakuwa muongozo wake. Hivyo wewe ndiye mwalimu wake namba moja. Hivyo kuanguka kwake itagemea na wewe lakini ukioa asiye na bikra huna utakachomfundisha kwani tayari msingi walijenga wengine. Hayo maelezo walishaelezaga wadau humu.

Ingawaje nampingaga Jokajeusi kuwa Bikra sio kila kitu lakini kwa umri wako kijana bikra inanafasi kwa zaidi ya asilimia 70


Mwanamke sifa yake kuu ni uzuri. Kuna Mwanamke alafu kuna Mke.
Kigezo cha uzuri katika kutafuta Mke hakitakuja kuondolewa kwa sababu huo ndio sababu ya Mwanamke kuitwa Mwanamke.
Lazima uoe Mwanamke mzuri. Inyeshe mvua Liwake jua. Achana na wale wanaoogopa Wanawake wazuri. Wakisingizia kuoa tabia njema.
Tabia njema ni sehemu ya seti ya lazima katika kuchagua mke lakini haiondoi sifa ya uzuri wa Mwanamke.
Lazima uoe mwanamke mzuri mwenye tabia nzuri.
Asije akakudanganya kuwa hao wanawake hawapo. Wanaosema hivyo ni waongo na usijifunze kwa Watu walioshindwa.
Hujawahi kuona Mtu fulani Mke wake ni mzuri, anatabia njema, anaelimu nzuri, na anafanya kazi yenye kipato?
Kama hujawahi kuona njoo nikuonyeshe.
Usisikilize maneno ya Watu walioshindwa ndio maneno yao hayo.


Sio kipato chako. Hapana kipato chake binafsi.
Kijana ukiwa katika umri huo. Lazima uchague Mwanamke mwenye sifa nilizotaja hapo juu na hii. Zote kwa pamoja.
Mwanamke kama hana kipato uzuri wake hauna maana yoyote kwako. Hakuamini kitu kizuri kikawa maskini, hakizalishi kipato na hakijitegemei. Hakuna uzuri wa hivyo.
Bikra, uzuri, kipato.

Mwanamke asiye na kipato huwaga namfananisha na nyumba isiyo na ghala la chakula. Lazima atakuwa tuu mnafiki, Malaya na mnyonyaji.
Mwanamke Mzuri, mwenye kipato na bikra mkikaa mnajadili vitu pasipo kuburuzwa.
Unauwezo wa kumuachia watoto wako na ukajua wako mikono salama.

Unaishi kwa raha. Sio ukiumwa kidogo unapata presha kuwa ukifa itakuwaje watoto watateseka.
Raha ya kufa ufe ukiwa na tumaini kuwa uliowaacha wako katika mikono salama ya Mwanamke anayejua nini chakufanya.

Ogopa Mwanamke asiye na kipato.
Ndoa itakuwa utapeli kama wadau dronedrake na wenzake wasemavyo.

4. Imani ya Mungu.
Mwanamke yeyote mwenye imani na Mungu anajua umuhimu wa kuolewa akiwa Bikra. Hiyo weka akilini kabisa.
Kwa umri huu huna haja ya kuuliza ilikuwaje huna Bikra. Swali hilo watauliza wakubwa zako wenye umri kuanzia miaka 36-50 hao ndio wanaruhusa ya kuoa Wasio na bikra.

2. Wanaume wenye miaka 36- 50
Hawa ni wakaka wakubwa na Wababa fulani hivi.
Hawa ndio wanaruhusa ya kuoa Wanawake wasio na bikra lakini hiyo haimaanishi waoe wanawake single Mothers(Yaani wenye watoto).

Vigezo vingine ni vilevile kama wenye miaka 20-35. Hawa tofauti yao ni kuwa wanaruhusiwa kuoa Wasio na bikra lakini wasiwe single Mothers.

3. Wanaume wenye miaka 51-85
Umri huu kila kitu kwenye maisha yako kitakuwa bayana. Yaani kama ni future yako itakuwa wazi machoni mwako.
Umri huu kama utahitaji kuoa basi unaruhusiwa kuoa Mwanamke Mwanamke asie na bikra na mwenye watoto ukipenda, pia waruhusiwa kuoa Mjane yaani Mwanamke aliyekwisha wahi kuolewa.

Zingatia; wakati unafanya jambo hili, uwe ushaweka mambo yako sawa kwa watoto wako ili baadaye isijeleta shida huko mbeleni. Kila mtu apewe kile anachostahili.

Hivyo ndivyo Watibeli tunavyofanya mambo yetu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
toa hicho kigezo cha kwamba mwanamke awe na kipato
 
Sawa tuanzie kwenye Bikra.
Kila mwanamke anazaliwa bikra si ndio?
Ila mazingira ndio yanapunguza au kuongeza chance ya hiyo bikra kuendelea kuwepo.

Binti akiwa mzuri chance ya ku survive na hiyo bikra hadi ndoa inapungua sana kwa asilimia kubwa. Unajua kwanini?? Kwa sababu nyie wanaume mkiona mtoto mzuri tu baaasiii, mnatumia mbinu zote za “kitibeli” mpaka muonje. Binti mzuri anazungukwa na vishaWishi vingi sana kuanzia shuleni (walimu) kwenye nyumba za ibada hadi mtaani. Kila mtu anataka aonje.

Unasema tena awe na kazii[emoji23][emoji23][emoji23]. Hapo uwezekano wa hiyo bikra kuendelea kuwepo ni ya kusaka kwa manati. Mabosi wenyewe ndio hawa hawa???[emoji23][emoji23][emoji23] Tena mtoto ni mzuri??

Wewe oa jobless tu
Ameandika vitu vizuri kwa kuviwaza lakini havina Applicability au ni very rarely case kutokea.

Yaani huyu binti mpaka amalize chuo lets miaka 20 apate kazi yaani bado hiyo bikra inakusubiri wewe

Mtibeli
 
Bikra + Mzuri + Mfanyakazi

Hii combination ni Moto yaan hapo unachochea kuni mwenyewe huku unajikaanga ukiwa juu ya chungu ongezea asiwe mpiga mizinga kinachowatiririsha UWABATA ni mizinga sio bikra sio uzuri sio ufanyakazi mizinga kabla haujaoa unapiga mahesabu gharama ulizotumia kumsotea kwenye vizinga zinazidi mahari uliyotajiwa na Baba yake

😄😄
 
Ameandika vitu vizuri kwa kuviwaza lakini havina Applicability au ni very rarely case kutokea.

Yaani huyu binti mpaka amalize chuo lets miaka 20 apate kazi yaani bado hiyo bikra inakusubiri wewe

Mtibeli
Tena Binti Mzuri … yaani “Mzuri”
 
Bikira utampata wapi...

Maana hata za sikio hamna siku hizi...
 
Awe bikra hapo hapo awe” mzuri” na awe na kazi (Kipato). Ningekuambia kitu ila basi tu.

Ila mnatukoroga sisi ma jobless, jana tu si mmetoka kusema mwanamke mwenye kazi ni mwanaume mwenzenu muoe ambaye hana kazi?

Amehlo tujipange upya sasa😂😂

Kumpata mwanamke bikra, mzuri na ana kipato inawezekana..

Ila mwanaume uwe high value man, uwe sehemu sahihi ya kukutana nao wanawake wenye sifa hizo, Na pia mwanaume usiwe mkubwa sana. Na mwanaume uwe umejipata

Wanawake wenye sifa hizo unawapata hasa wale ma Auditor wa PWC, KPMG, Dellote na Ernest young.

Ukiwa unafanya kazi kampuni kubwa yoyote lazima uwe unaviona hivi vidada vya hizi kampuni nilizozitaja vikija ku audit ofisini kwenu.

Ama mwanaume na wewe upate kazi kwenye hizo kampuni za audit. Utajuana navyo vingi na kupata mmojawapo wa kumuoa.

Hivi vibinti asilimia 90 vinaajiriwa bikra. Maana kwanza vinapata ajira mapema chuo vinamaliza mwezi wa 7 na kazi wanaanza mwezi wa 9. Kabla ya graduation vinakuwa kazini tayari.

Sababu kwanza vinakuwa best student udsm, Udom ama Mzumbe. Best students wa kike ngumu sana kujihusisha na mahusiano. Maana chuo vinasoma kozi ngumu ngumu. Za engineering ama B com Accounting

Pili sekondari vinakuwa vimefanya sayansi combination na vimepiga div one Point kali.. binti wa PCM ama PCB ngumu sana kujihusisha na mapenzi.
Shule zenyewe wanasoma zisizo na vishawishi kama St Francis, Marian, Mazinde Juu,

Hawa asilimia kubwa wanaolewa na bikra zao.
 
Sawa tuanzie kwenye Bikra.
Kila mwanamke anazaliwa bikra si ndio?
Ila mazingira ndio yanapunguza au kuongeza chance ya hiyo bikra kuendelea kuwepo.

Binti akiwa mzuri chance ya ku survive na hiyo bikra hadi ndoa inapungua sana kwa asilimia kubwa. Unajua kwanini?? Kwa sababu nyie wanaume mkiona mtoto mzuri tu baaasiii, mnatumia mbinu zote za “kitibeli” mpaka muonje. Binti mzuri anazungukwa na vishaWishi vingi sana kuanzia shuleni (walimu) kwenye nyumba za ibada hadi mtaani. Kila mtu anataka aonje.

Unasema tena awe na kazii😂😂😂. Hapo uwezekano wa hiyo bikra kuendelea kuwepo ni ya kusaka kwa manati. Mabosi wenyewe ndio hawa hawa???😂😂😂 Tena mtoto ni mzuri??

Wewe oa jobless tu

Binti anakuwa affected na mazingira

Ukienda shule kama marian kwa mfano, ama st francis sio ajabu kukuta darasa zima la form 4 limejaa bikira.

Lakini ukienda shule za kata ama shule za Dar mfano jangwani girls. Unaweza usimpate bikra hata mmoja kwenye darasa hilo hilo la form 4.
 
Enhee sijaamini kama nishakuwa jimama 🤣

Kuhusu mada ya mtibeli, hivyo ndivyo inavyotakiwa, unfortunately mambo hayatokei katika mstari ulionyooka. Mambo kwa ground yanatokea kibahati bahati tu na vigezo fulani fulani. Wanaume wote wakifuata vigezo vya mtibeli mdada wa sasa kuolewa chances are nill.
Tushakua majibaba na majimama😁
 
Nakazia , oa mwanamke ambae mama yake anatambua umuhimu wa baba katika familia.

Usioe mtoto wa feminist kamwe, ambae baba yake hana sauti kwenye familia.

Note: kukataa ndoa ni bora zaidi.
Nadhani matatizo yote yanaweza suluhishika ila hili ulilosema kamwe abadan halisuluhishiki..
'' Kijana ogopa sana kuoa mwanamke ambaye mamaake ana sauti kuliko babake ake"
Ogopa mnoo.
Bora singlemom alieefiwa na bwana alomzalisha kuliko mwanamke ambae kwao mama ndo ananguvu.
 
Mbona kama umekata tamaa mkuu😄😄
Ni mziki si wa kitoto kaka maana hizo sifa ulizoainisha dunia ya leo haziendi sambamba,
Ukiona mwanamke mwenye kipato ujue wamemtoboa sana kufika hapo, Na ukiona Bikra automatically ni mdogo hivyo economically dependent.
Na sasa case ya urembo hapa unakuta katobolewa haswahaswa hata kama ana kipato.
 
Ni mziki si wa kitoto kaka maana hizo sifa ulizoainisha dunia ya leo haziendi sambamba,
Ukiona mwanamke mwenye kipato ujue wamemtoboa sana kufika hapo, Na ukiona Bikra automatically ni mdogo hivyo economically dependent.
Na sasa case ya urembo hapa unakuta katobolewa haswahaswa hata kama ana kipato.

Kwisha habari yenu.
Yaani hapa ni kukata tamaa kabisa
 
Back
Top Bottom