Vijana ili uhesabiwe mwanaume ni lazima uoe

Vijana ili uhesabiwe mwanaume ni lazima uoe

Dah!..hongera sana aisee, wapo tunaotamani hivyo ila sasa...
Mkuu nilipotangaza kuoa,wapotoshaji wakaanza kujileta mara ooh ndoa si lele mama wakaanza kunitolea mifano ya ndoa zilizoyumba mpaka ya Mandela.Nilisikiliza ushauri wao nikachanganya na zangu nikaoa.
Huwezi amini walewale wakionipotosha ndio yakiwakuta kwa mahawara zao wanakimbilia kwangu
OA mkuu ili ukue tuwaongoze wadogo zetu
 
1. Je mapadri sio wanaume halisi?

2. Je ni kifungu gani cha bilblia kina LAZIMISHA watu wao au waolewe?

3. Je kifungu gani cha katiba kinalazimisha mtu aoe au aolewe?

4. Sisi kama wakristo tuna fwata mafunzo ya Yesu na mitume wengine kama mtume Paulo.

Lakini kiuhalisia ni kwamba hawakuoa je nao unawasemeaje?

NB: Naomba unijibu maswali yote.
Endelea tu kuzini mkuu...kwani Kuna shida ?
 
Mwanaume amezaliwa kiongozi hivyo yako ikiwa fasheni inabidi uvae uanaume wako,onyesha njia mkeo atafuata hata kama mkeo ni waziri
Tena huko ulikoongea ndio kabisa. Mkeo awe waziri au mbunge uwe tu tayari kumuacha,mwanamke kwamba wewe utamlazimisha afuate sheria zako hapo tayari ameshakuwa waziri?. Vinginevyo atafuata kabla hajafikia hiyo ngazi.
 
Mkuu wengine tumeoa na mambo yakazidishiwa baraka..maneno yako yatazidi kuwaharibu
Haya nyie endeleeni kuwadanganya vijana,

Yaan kijana uchumi haujasimama kwa miguu miwili ,unataka aoe eti atakua stable akishaoa ....daaah hii theory ya uchumi sijui ni ya sayari gani
 
Ukioa ndo unapata Baraka. Unaweza fanya yote hayo kirahisi na kifanisi ukiwa ndani ya ndoa.
Jidanganye tu..

Yaan uwe na kipato cha mfano million moja then ushindwe kununua IST ukiwa mmoja then ununue mkiwa wawili na zaid(familia yenu, yako na yake) hii hesabu ya wapi mkuu....usiniambie eti ukioa fursa zinaongezeka,hizo huwa ni coincidence tu
 
Hahahah labda uwe na mke fighter akubali kuchangia maendeleo kwa hela yake.
 
Yaani hawa ndio wanapotosha vijana.Safi sana mkuu,hivi fikiria raha tunayopata tuliyooa upo mezani na mkeo na watoto meza imesheni vinono,angalia watoto wako wavyofurahi na kuwaangalieni kwa jicho la upendo.
AU ona unavyotoka na familia yako shopping mke pembeni yako watoto nyuma yenu,
ETI mtu hajaoa halafu anadai anakula maisha,kula maisha umezungukwa na makahaba!! OENI MFAIDI

Kama huna hela hizi zitabaki kuwa lucid dreams
 
Kukariri mambo kwa hii dunia tunayoishi sasa ni kujifelisha vibaya mno! Ufanye jambo kisa baba au mama alifanya utajikuta unaangukia pua...
Kwa akili yangu fupi uwezi kunambia ili niwe mwanaume niliye kamilika lazima niwe nimeoa...
 
Hahahah labda uwe na mke fighter akubali kuchangia maendeleo kwa hela yake.
Kwa wanawake hawa wa 50/50 kwenye haki ila kugawanya majukumu 100/0 na ile kauli mbiu yao ya chako chenu chake chake....hiyo ni ndoto ya mchana
 
Kukariri mambo kwa hii dunia tunayoishi sasa ni kujifelisha vibaya mno! Ufanye jambo kisa baba au mama alifanya utajikuta unaangukia pua...
Kwa akili yangu fupi uwezi kunambia ili niwe mwanaume niliye kamilika lazima niwe nimeoa...
Hawa jamaa wanaleta theory za decades back katika ulimwengu huu wa leo,bila kusahau kila kitu kimebadilika na kuna changamoto nyingi mpya za ulimwengu wa leo ambazo ukitaka kuzi solve kimazoea utachelewa sana au utaangukia pua
 
Endelea tu kuzini mkuu...kwani Kuna shida ?

Mkuu hata huko kwenye uzinifu hawana furaha kabisa,hata threads zao wanazoleta humu utagundua,mwisho wanaishia kutukanana mara sijui vibamia sijui bwawa
HAPANA waoe tu!
 
Naona bado haujakutana na hawa viumbe. Usipotumia hekima na busara. Jela inakuhusu
Huyo uliyempata katulia kwako, basi unaona kama wanawake wote wanafanana na wa kwako kitabia, sura mpaka umbo. Kwahiyo unafikiri mwanamke ni malaika (hana madhaifu)?.
Utakuwa umeoa mwanamke aliyezaliwa 1970 kushuka chini
Ukiona hupati utulivu kwenye ndoa jitathimini uanaume wako
Kuna mtu alileta uzi 'KAMA NDOA IKIVUNJIKA MWANAUME NDIO WA KULAUMIWA'
yupo sahihi mkuu
 
Hawa jamaa wanaleta theory za decades back katika ulimwengu huu wa leo,bila kusahau kila kitu kimebadilika na kuna changamoto nyingi mpya za ulimwengu wa leo ambazo ukitaka kuzi solve kimazoea utachelewa sana au utaangukia pua
Kumbuka mwanaume ndio kiongozi wa ulimwengu huu,moja ya sifa ya mwanaume ni kuzikabili changamoto na kuzishinda
Mkuu vuta mke oa sio kuwaogopa hawa wameletwa kwa ajili yetu tusaidiane kuujenga ulimwengu
 
Naona bado haujakutana na hawa viumbe. Usipotumia hekima na busara. Jela inakuhusu
Huyo uliyempata katulia kwako, basi unaona kama wanawake wote wanafanana na wa kwako kitabia, sura mpaka umbo. Kwahiyo unafikiri mwanamke ni malaika (hana madhaifu)?.
Utakuwa umeoa mwanamke aliyezaliwa 1970 kushuka chini
Mkuu wangu kazaliwa 1984,bado mbichi na nimemsomesha(kitu ambacho hamtaki kukisikia),
 
Hawa jamaa wanaleta theory za decades back katika ulimwengu huu wa leo,bila kusahau kila kitu kimebadilika na kuna changamoto nyingi mpya za ulimwengu wa leo ambazo ukitaka kuzi solve kimazoea utachelewa sana au utaangukia pua
Kabisa! Na ukioa ili kuonyesha wewe ni mwanaune mbele ya umma, jua uko na shida pahala..
 
Back
Top Bottom