Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Una umri gani?

Kama ni mtu mzima unajishughulisha na nini?
MIMI Nina umri wa mtu Mzima sana naweza nikawa nakuzidi au tunalingana kiumri kuhusu shughuli yangu hio sijajua unataka kufahamu kwanini na inahusiana nini na hii Mada lakini kwa kukusaidia ninafanya biashara pia za hapa na pale yaan in & out sio permanent hapo nadhani umenielewa sasa nijibu swali langu
 
Jawabu la swali lako katizame series inayoitwa The Gentlemen. Netflix ipo utaipata kwa urahisi.

Majibu ya maswali yako yote yapo humo!
 
Kumbe story ni nyingi sana tamaa mbele Mauti nyuma
 
Milionea wa wiki 2😀😀😀😀😀
 
waliochochea migomo na wanaoongea vibaya kumhusu mtu fulani wanaanza kushughuliwa taratibu na wapumbavu
 
wapinzani bongo miyeyusho sana,wanafanya sometimes tunaona bora hawa majini wetu waliomadarakani..
nilishangaa sana kuona zile kelele nyingi vile nikasema hawa jamaa wanawafahm vizuri hawa watu wanaowapigia kelele wapatikane
Watu wenye mawazo kama yako wanasumbuliwa na ujinga. Huwezi kuwa na nchi yenye serikali inayoua watu kwa siri hata kama ni majambazi. Unajua madhara yake? Bila shaka hujui.
 
Yupo kama mtoto
Ndiyo maana nimempatia series moja inaitwa the Gentlemen. Inaonyesha jinsi matajiri wanavyoishi na kuendesha biashara zao nje na vile jamii inavyojua.

Pia inaonyesha namna gani ukileta magumashi wanavyokupoteza bila kusita.

Kwenye biashara watu wanalinda jina/uamnifu na Kingdom yake. Huwezi ukaleta ujuaji kwenye kimojawapo halafu wakakuacha.

Mfano mzuri kipindi cha JK: Kampuni moja ya clearing and forwarding kwa ghafla tu ilikuwa juu kuliko kampuni nyengine. Walianzisha na ofisi yao China hivyo ikawa inawadaka wafanyabiashara wa Tanzania hukohuko na huku wana kampuni yao.

Matokeo kampuni nyengine zikawa zinakosa kazi na zinakufa. Kilochotokea Mkurugenzi mtendaji wa hiyo kampuni siku yupo Kariakoo kwa ghalfa mtu kamgusa nyuma kwenye bega. Ile kugeuka tu kamwagiwa tindikali usoni. Za chini chini zikawa zinasemwa kwamba wafanyabiashara wenzake waliona watakufa njaa haiwezekani mtu mmoja atawale biashara nzima wao watakula wapi!

Hivyo biashara zina umafia sana chini ya kapeti. Watu wapo serious na kazi zao. Watu wanachukua mikopo na wakati mwengine pesa wanazipata kwa njia zisizo halali halafu uzingue! Wanakupoteza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…