Ni kweli UTI ni ugonjwa hatari unashambulia maeneo matatu njia ya mkojo, kibofu na figo. Kila eneo lina aina mahususi ya bakteria wanaoleta athari.
Hatari huwa kubwa zaidi wakishambulia kibofu au figo, njia za kupata UTI ni nyingi mfano kuingia kwa haja kubwa kwenye njia ya mkojo hasa wanawake wakati wa kujifuta baada ya haja (inashauriwa anzia mbele kurudi nyuma) na watoto wanaovalishwa diaper mnaita pampas, wanaojamiana kwenye njia ya haja kubwa pia matumizi ya vifaa vya kuzuia mimba, matumizi ya muda mrefu ya antibiotic, kutokunywa maji kwa wingi, ukomo wa hedhi, matumizi ya catheter, kutokumalizika kwa mkojo baada ya kukojoa inawezekana kwa sababu ya tezi dume au mawe kwenye figo, kuwa na kisukari, matumizi ya vyoo vichafu nk. So umakini uanzie hapa.
Pia jitahidi sana kukojoa mara tu baada kumaliza kujamiana... kunywa maji mengi. Usitumie mate kama kilainishi wakati wa tendo... unahamisha bacteria na kuibua maambukizi.