Vijana mnakwama wapi? Kuna kijana nilimuunganisha ajira hata asante hajanipa anataka nimtafutie ajira sehemu nyingine sasa

Vijana mnakwama wapi? Kuna kijana nilimuunganisha ajira hata asante hajanipa anataka nimtafutie ajira sehemu nyingine sasa

tenda wema nenda zako usingoje shukrani
ila watu wa kusini ndivyo hulka zao ukimpa kitu au msaada hawezi sema asante
anaona kama ni halali kwake kupata hicho alichokitaka kutoka kwako na ni stahiki yake
Kama umewahi kuishi kusini au kuishi na watu wa kusini unajua nini nazungumza hapa.
Watu wa kusini hata kuomba hatujui.
Utasikia mjomba una pesa nirushie tigopesa?
Unakasirika muda mwingine unafanya tu kwakuwa ni ndugu
 
Afadhari wewe huyo uliemsaidia bado yupo kazina na hakuna kashifa yeyote ili iliyotokea, sasa mimi nilimpambania mtoto wa dada binamu ktk ukoo na ukizingatia elimu yake ni fomu 4 mwenye D 2 na akapata kazi nzuri tu mshahara laki 5, lakini cha ajabu kaenda kazini siku mbili tu na kuacha kazi hadi dada (mama yake mzazi) alidondosha kilio na machozi baada ya kuona binti yake kagoma kwenda kazini.

Leo hii nimepita ktk kampuni fulani wameniomba niwatafutie mfanyakazi nikakimbuka lile sakata nikasema moyoni simtafutii tena mtoto wa mtu kazi nilikumbuka issue ya yule binti alivyonidhalilisha baada ya kuacha kazi.
Hawa vijana wakike na wakiume mostly ni wajinga sana
Sasa mtu kakuhangahikia halafu anaacha kazi. Alijua huko kazini ni kunywa supu na chapati basi anasubiri mshahara?
 
Kama umewahi kuishi kusini au kuishi na watu wa kusini unajua nini nazungumza hapa.
Watu wa kusini hata kuomba hatujui.
Utasikia mjomba una pesa nirushie tigopesa?
Unakasirika muda mwingine unafanya tu kwakuwa ni ndugu
nawapatavizuri
chake ni chake
chako chake na ukimnyima utageuzwa matangazo
 
Kama anafanya vizuri na ajakuaabisha msaidie tu, kwani wema uliomfanyia ulikuwa na makubaliano ya malipo?

Alipaswa akushukuru kama unavyosema na kg ya sukari, ila asipofanya hivyo haliwi kosa au sababu ya kutomtendea wema.

Sio wote wenye huo ufaham, tumelelewa tofaufi na mazingira tofauti, tenda wema kama hatokuaibisha, kuna mtu atawatendea wema wanao huko mbele.
Siyo kila king'aacho ni dhahabu. Kuna watu wanalipwa kiduchu,ila mazingira safi. Kuna wengine wanapokea kiasi kikubwa,ila mazingira magumu.
Siku zote ukisahau ulipokuwa,yanakuwa hivi hivi.
-Kwa nini anataka kuhama?
-kwa nini alipopata taarifa, wasiendelee kumpigania?

Kuna msemo mmoja, kwamba mbwa hukumbuka umhimu wa mkia ukishakatika
Sijamtukana mtu hapa. Lakini,kuna watu akishika tu kitu,hashikiki,mpaka apinde ndo utamuona. Kwa kiasi hicho, hata angechukua mchele,mafuta na unga akapeleka kwenye familia ya jama,ingekuwa shukrani tosha.
Huenda hata mawasiliano alikata.
 
Wewe wa hovyo sana ungenyamaza tuu. Dunia hii kumuunganisha mtu kazini ni jambo la kuhitaji malipo? Huyo dogo moyoni anakuona kama mkubwa wake ndiyo maana kakukumbuka tena.
Wapi kadai malipo?
Uendapo hotelini au kwa ma ntilie,si unakula/kunywa na unalipa!! Lakini ukiaga, si unashukuru!
Kinashindikana kitu gani kumuonyesha alokusaidia kwamba unathamini mchango wake? Shukrani si pesa tu. Hata kitu chochote unaweza kinunua,ukampa mtu.
Pata pesa tujue tabia yako. Sasa,kama huna shukrani,unaweza msaidia mwenzio? Anaesaidia mwenzie,na anayetambua uchungu wa kupigika
 
Huyu kijana kafeli sana vyovyote vile shukrani kwa mtu aliyekutoa juu ya mawe ni lazima na ndio ustaarabu.

Aisee mie shida yangu nadaiwa direct cost Tsh 243,750 nipo udom hapa semister inaenda kukata sielewi na sijakamilisha usajili noma....

Control number 994461469086
Inasikitisha Sana upo University lakini akili huna.

Hujui hata how to approach kuomba msaada, huko vyuoni mnafundishwa ujinga au ni nini hasa?

Hivi hata mtu kama pesa yake haina kazi ndio itoke Kwa style hii kweli.

Mimi roho inaniuma Sana nikiona kijana University level halafu bado mjinga na hajitambui.
 
Kama anafanya vizuri na ajakuaabisha msaidie tu, kwani wema uliomfanyia ulikuwa na makubaliano ya malipo?

Alipaswa akushukuru kama unavyosema na kg ya sukari, ila asipofanya hivyo haliwi kosa au sababu ya kutomtendea wema.

Sio wote wenye huo ufaham, tumelelewa tofaufi na mazingira tofauti, tenda wema kama hatokuaibisha, kuna mtu atawatendea wema wanao huko mbele.
Mchango Bora kabisa
 
Hello!
Huyu dogo kama atakuwa humu atasoma bandiko hili maana si baya kivile.
Imepita mwaka sasa tangu nimuunganishe kwenye ajira (sekta binafsi) kama dereva wa malori. Kampuni kubwa tu hapa Bongo. Anapokea around 500k -800k kwa mwezi.
Sasa ile stori na wenzake anapata kujua fursa zaidi kwenye kampuni zingine.
Si unajua stori za wafanyakazi kupenda kuambiana sehemu B wako vizuri kimaslahi.
Lengo langu si kutazamia malipo kwake, nilimsaidia tu , kilichonishangaza bado anataka tena connection kutoka kwangu anashindwa kujisimamia afike huko anakowaza.
Sasa akisikia kuna sehemu wanalipa vizuri zaidi ananipigia simu kutaka nimuunganishe ajira huko.
Mtu alikuwa juu ya mawe umemfanyia mpango hajakumbuka hata ile brother Asante kilo ya sukari hii hapa unywe chai na watoto leo anataka umpigañie sehemu nyingine.
Ikumbukwe huyu dogo hatuna undugu , nilidanhanya ni mtoto wa dada yangu ili apate ajira maana ningesema mdogo wangu majina yangeumbua.
Sikuhitaji malipo, nilikuwa nikimpa kampani ndogo ndogo kabla hajaajiriwa. Hata alipoajiriwa kuna siku alikwama akaomba nimkopeshe pesa kidogo atalipa mwisho wa mwezi. Nikamtumia pesa zaidi ya aliyohitaji na nikamwambia siwezi kukukopesha nakupa tu free, si vyema tuishi maisha ya kukopana fedha. Leo kanitext nilijua anataka anishukuru arudishe kiutu uzima ile pesa niliyomtumia kumbe anataka nimpigabie ajira ofisi fulani ya umma.
Nadhani hii tabia ya kutojielewa sijui ni mazao ya origin ya mtu. Watu wa kusini shukrani kwetu ni kitendawili.
Ok . Badala ya kujipambania sasa unataka ubebwe tena.
Note: Mimi si dalali wa ajira na sihitaji pesa ya mtu . Nimezungumza tu kijana lazima uwe na akili timamu katika utafutaji wako wa maisha.

Kutoa fadhila ni jambo la hiari wala sio lazima.

Kama umemsaidia akapiga hatua fulani kwenye maisha ni jambo jema lakini si lazima upewe shukrani maana huo ni moyo wa mtu.

Usiwe na roho dhaifu kiasi hicho mpaka kuja kumuanika kwenye majukwaa kwa sababu fadhila sio kitu cha lazima au fidia.
 
Hello!
Huyu dogo kama atakuwa humu atasoma bandiko hili maana si baya kivile.
Imepita mwaka sasa tangu nimuunganishe kwenye ajira (sekta binafsi) kama dereva wa malori. Kampuni kubwa tu hapa Bongo. Anapokea around 500k -800k kwa mwezi.
Sasa ile stori na wenzake anapata kujua fursa zaidi kwenye kampuni zingine.
Si unajua stori za wafanyakazi kupenda kuambiana sehemu B wako vizuri kimaslahi.
Lengo langu si kutazamia malipo kwake, nilimsaidia tu , kilichonishangaza bado anataka tena connection kutoka kwangu anashindwa kujisimamia afike huko anakowaza.
Sasa akisikia kuna sehemu wanalipa vizuri zaidi ananipigia simu kutaka nimuunganishe ajira huko.
Mtu alikuwa juu ya mawe umemfanyia mpango hajakumbuka hata ile brother Asante kilo ya sukari hii hapa unywe chai na watoto leo anataka umpigañie sehemu nyingine.
Ikumbukwe huyu dogo hatuna undugu , nilidanhanya ni mtoto wa dada yangu ili apate ajira maana ningesema mdogo wangu majina yangeumbua.
Sikuhitaji malipo, nilikuwa nikimpa kampani ndogo ndogo kabla hajaajiriwa. Hata alipoajiriwa kuna siku alikwama akaomba nimkopeshe pesa kidogo atalipa mwisho wa mwezi. Nikamtumia pesa zaidi ya aliyohitaji na nikamwambia siwezi kukukopesha nakupa tu free, si vyema tuishi maisha ya kukopana fedha. Leo kanitext nilijua anataka anishukuru arudishe kiutu uzima ile pesa niliyomtumia kumbe anataka nimpigabie ajira ofisi fulani ya umma.
Nadhani hii tabia ya kutojielewa sijui ni mazao ya origin ya mtu. Watu wa kusini shukrani kwetu ni kitendawili.
Ok . Badala ya kujipambania sasa unataka ubebwe tena.
Note: Mimi si dalali wa ajira na sihitaji pesa ya mtu . Nimezungumza tu kijana lazima uwe na akili timamu katika utafutaji wako wa maisha.
Unazinguka sana dingilahi ukweli ni kuwa unahitaji hela yake ya ahsante kwako .

Anyway mpe shavu kama lipo kesho yako inaweza kuwa mikononi mwake .

Nimemkumbuka rafiki yangu Nyafwili ukimuona mwambie dokta wa kijiji cha wagagikoko anamsalimia sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
"Sasa mtoa mada ananizungumzia mm hapa. Sasa Kwa taarifa yako sikupi cha shukran wala hata mia huonji na hii hela siirudishi...ww mbona serikali imekupambania ukiwa mdogo kadi yako imejaa ushauri sijui upewe ugali wa mtama mara ule nyama ya dog! Kama haitoshi ukasoma na mkopo bado ukaajiriwa vp uliwahi peleka shukran serikalini"

Brother huyo dogo kama yupo humu atakujibu hvo
 
Habari za siku nyingi MENEMENE TEKERI NA PERESI , wanasemaje hapo kwa wagagikoko..
Anhaa sikuoni ndugu yangu au kuna corridor sipiti ?
Hapa ni wazima wa afya tuko na ligi ya kijiji bingwa anapewa suruali ya kitambaa kwa kila mchezaji hivyo wikiendi yangu inaishia hapa uwanjani maana leo ni fainali .

Niko natizama fainali huku nanyonya taratibu pombe yangu ya kienyeji ya "DADII"

Bila kusahau ndugu yetu mwandishi wa michezo anayetoka huku kwetu tuko naye hapa bwana Baraka MPENJA na mimi nimepewa heshima ya kukaa naye meza kuu hapa kwenye siti za mbao ndefu .

Actually wikiendi imefana Nyafwili

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom