Vijana mnakwama wapi? Kuna kijana nilimuunganisha ajira hata asante hajanipa anataka nimtafutie ajira sehemu nyingine sasa

Vijana mnakwama wapi? Kuna kijana nilimuunganisha ajira hata asante hajanipa anataka nimtafutie ajira sehemu nyingine sasa

Asante ni neno kubwa sana.

Kuna wakati unasaidiwa pakubwa hadi unapagawa ni kwa namna gani unaweza kushukuru.

Ukipiga hesabu za manufaa uliyoyapata unashindwa utoe kiasi gani kumshukuru aliyekusaidia.

Inawezekana kijana yupo katika hali hiyo ila kumbe wewe upo mtandaoni kumlaumu.
Nimejifunza kitu
Watu wengi hawajui Mungu Huwa anawaweka mahali Ili kuwa msaada Kwa watu wengine!
Kushukuriwa ni vzr, lkn Mungu ndo Huwa anatoa shukrani za ukweli
Utashangaa Kwa kuwasaidia hao watu Mungu anakufungulia na we milango,mambo Yako yanaenda ...
Kumbe yule uliyemsaidia,anamshukuru Mungu Kwa ajili Yako anakuombea Mungu akuinue zaidi.....

Hii ni nzuri kuliko ht pesa
 
Nimejifunza kitu
Watu wengi hawajui Mungu Huwa anawaweka mahali Ili kuwa msaada Kwa watu wengine!
Kushukuriwa ni vzr, lkn Mungu ndo Huwa anatoa shukrani za ukweli
Utashangaa Kwa kuwasaidia hao watu Mungu anakufungulia na we milango,mambo Yako yanaenda ...
Kumbe yule uliyemsaidia,anamshukuru Mungu Kwa ajili Yako anakuombea Mungu akuinue zaidi.....

Hii ni nzuri kuliko ht pesa

Ni kweli.

Kutoa msaada ni moja ya njia ya kufungua milango ya baraka kwa sababu kiendacho hurudi.
 
Hii imenikumbusha, niliishi na watoto wa bro, kuanzia form 1-4, siyo kwamba bro hayupo, yupo na aliomba kwasababu ya ubora wa shule zilizopo nikakubali bhana, wanapishana madarasa na walikuwa watatu. Akaja mtoto wa shemeji yangu naye nimeishi nae form 1-4. Walikuwa wanasoma boarding schools, tofauti tofauti japokuwa chochote shuleni mie ndo naenda, kipindi Cha likizo lazima niwe nimejipanga, adolescence ikawakutia kwangu nk. Sikuacha kuwahudumia kadiri tulivyojaaliwa.

Watoto wote walitoka na ufaulu safii kabisa wakaenda kukichafua sana huko mikoani kwao. Tangia waondoke, kama nilipokea hata simu ya mtoto huyu kafika salama, huyu kafika! HAKUKA JAMAN HAKUNAAAAAAA! Ile kusema tu Asante maana sihitaji chochote HAKUNA.

Juzi kati wanaomba walete mtoto wa form 1 tena nikasema tu HAPANA wapendwa siko tayari kuchuma dhambi ya manung'uniko. Cheki na ndugu wengine wasaidie hapo.

Tujifunze kusema ASANTE, maana yake ni rahisi kurudi na kuomba tena na usikose!
 
Huu msemo wa tenda wema nenda zako kuwa careful nao, kuna dogo miaka kadhaa nyuma nilimsaidia akapata kazi nzuri tu , qualifications zake hazikuwa proper ila mpaka kuhonga nilihonga ilimradi dogo apate, kweli alipata ila alipoingia tu ndo visanga vilianza .Kijana alinisema vibaya sana kule zile taarifa boss wake ndo kaniletea , ikumbukwe boss ni miongoni mwa waliokula rushwa na simu zisizoisha ndo dogo yule apate kazi ,alishangaa sana .
Two years later alishikwa na sakata la wizi , walifutwa kama 25 hivi waliokuwa wanapiga lile deal .
Sasa ndio dogo alinikumbuka,alikuja na pole nyingi sijui nini ila sikutaka hata kuskia.
Ukisaidiwa kumbuka kurudisha fadhila hata kama aliyekusaidia hayupo uhai, peleka shukrani kwa familia yake .
Aliyenishika mkono na kunitoa mpaka leo tunaukaribu mkubwa sana , sipiti siku mbili tatu bila kumcheki hali
Fadhila muhimu tena sana
 
Afadhari wewe huyo uliemsaidia bado yupo kazina na hakuna kashifa yeyote ili iliyotokea, sasa mimi nilimpambania mtoto wa dada binamu ktk ukoo na ukizingatia elimu yake ni fomu 4 mwenye D 2 na akapata kazi nzuri tu mshahara laki 5, lakini cha ajabu kaenda kazini siku mbili tu na kuacha kazi hadi dada (mama yake mzazi) alidondosha kilio na machozi baada ya kuona binti yake kagoma kwenda kazini.

Leo hii nimepita ktk kampuni fulani wameniomba niwatafutie mfanyakazi nikakimbuka lile sakata nikasema moyoni simtafutii tena mtoto wa mtu kazi nilikumbuka issue ya yule binti alivyonidhalilisha baada ya kuacha kazi.
Afadhali ww mkuu , nilinuunganisha dogo flani wa kijijini kazi , yule aligeuka mwizi kule . Aibu iliyonipata stowai sahau
 
Back
Top Bottom