Tusiishie kulaumu wanawake Tu, tukubaliane na uhalisia kwamba miongoni mfumo wa maisha tulio upokea kwa jina la utandawazi Una mchango mkubwa katika kutikisa taasisi ya ndoa, watu wanaingia kwenye ndoa kupitia lifestyle za wenza wao wanazoziona kwa juu juu Tu ama mitandaoni, mtu huna background ya familia yake mnakutana ki mjini mjini mnaingia kwenye mahusiano baada ya mapenzi kuwanogea mnatangaza ndoa, kwa mtindo huo kutoboa ni bahati nasibu.
Mmekutana kwenye early 25's ama 27's zenu, mna background tofauti, mnaficha tofauti zenu ili mfikie lengo la ndoa ili kukwepa presha kutoka kwenye familia au jamii zinazowazunguka, mkishaingia kwenye ndoa kila mtu anaanza kutoa makucha yake sasa, mwingine kwao wana asili ya kuamini imani za kishirikina mkishaingia kwenye ndoa ndio anaanza rasmi kugeuza nyumba yenu kama uwanja wa majaribio, mwingine kwao wana asili ya kiburi akisha ingia kwenye ndoa ndio anaanza kukuonyesha vizuri kiburi chake.
Kutokana na mabadiliko ya ki mfumo wa maisha ndio maana hao waliotuletea utandawazi walikuja na aina tofauti tofauti za ndoa, ndoa za mikataba, ndoa za open relationship etc.
Ukiangalia jamii zilizokataa kuingia kwenye mfumo wa utandawazi utaona hata rate ya talaka ni ndogo sana kwao.