Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

hao vijana wamelala kazini kama ambavyo manesi wanalala kazini kama ambayo polisi wanalala kazini nyani haoni kundule social media pia inalemaza akili, ukikutana na mfanya biashara atakwambia ajira inakudumaza uwezo wako wa kufikiri, utakutana na mwanamke ambae hafikirii maendeleo naye atakulemaza akili, utakutana na mtu anakwambia ukikaa kijijini akili italemaa, mwingine atakwambia kuangalia mpira kutakulemaza akili hutafikiria vitu vya muhimu, maisha buana popote pale utachanganyikiwa kama wewe ni wakuchanganyikiwa.
 
Kuna makala hapa JF ya wacheza mpira maarufu huko Ulaya, waliolipwa mabilioni ya fedha, baada ya kustaafu wamefilisika kabisa, wamepanga hadi vyumba vya kuishi sababu ya kubet, endeleeni kusema Ni sayansi
 
Hahahahah kindege kikapagawa🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
AVIATOR SIO BETTING MKUU, HIYO NI LUCKY DIP, KUBET NI KWENYE MICHEZO AMBAYO MATOKEO YAKE YAPO WAZI MWISHO WA MCHEZO NA HAYAPANGIKI KWA PROGRAM ZA KOMPUTA. ULICHOFANYA WEWE NI KAMA UMECHEZA BIKO AU TATU MZUKA AU HII MICHEZO YA REDIONI YA KUTUMA 1000 USUBIRI HELA. AVIATOR INAWEZA KUWA NA ALGORITHM INAYOANGALIA UMEWEKA KIASI GANI ILI IKIHESABU IISHIE WAPI IPAE. NDI MAANA UKIANZA UNAKULA UKIENDELA UNASHANGAA UNAPOTEZA ILA UKIACHA ROUND IPITE HUJAWEKA DAU UNAONA INAHESABU MPAKA 2000 HUKO, UKITIA MZIGO TU INAISHIA 1.87 INAPAA. OGOPA MICHEZO YENYE PROGRAM YA KOMPUTER, NI LAZIMA KUWE NA NAMNA YA KUCHEKI FAIDA KWANZA KABLA HAWAJARUHUSU MTU ALE PESA NYINGI.
 
Ungenitafuta mapema ningekupa mbinu kiongozi aviator usipojua ni rahis kupoteza pesa yako. DM me
 
Ilibaki kidogo nianze kucheza kindege jamaa alisema atanifundisha
 
Ulifanyaje mpwa πŸ˜€
 
Weka picha za hicho kitoto chenye neema za Allah kama zote, tuone kama 5M imeenda kihalali.
 
Ilikuaje? Mbona wewe ni mjanja
Kwenye utabiri, hakuna ujanja kwa kweli, ile michezo inachezwa na binadamu, una calculate unaona hapa kuna goli, hapo zinakuwa piga nikupige, imegonga post, kipa kadaka, mtu kabaki na goli kapata kifafa kaanguka.

Kuhusu ujanja why nibet kiasi hicho na niliwe, addiction mchezo ule una addiction ya kifala sana, nilivyoanza na kufikia huku hayaelezeki ni kama utani tu, kisha inakuchota, ila niliacha baada ya kujifanyia tafakuri vizuri.
 
Yeah inawezekana kabisa kuacha kubeti ikiwa utaamua kutoka moyoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…