Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

Hatuachi kubeti Jana nimeanza na 30,000 tu kubeti kwenye soka Sasa hivi usiku huu Nina 200k ,unaniambiaje nibeti we utakuwa junior kwenye kubeti pia hauwezi zuia hisia na haujui betting inaendaje,na unaendaje kushindana na computer,betting zote izo aviator na virtual games ni computer ata siku Moja hauwezi shindana nazo
Tangu nijue uhuni unaoendelea virtual betting, Huwezi nishawishi kutia stake uko
 
Kama umebeti hadi kuliwa 7m ulistahili na kufukuzwa kazi. Bila shaka ni mtu wa hovyo job.
 
Jipige kifuani mara3 kisha utamke maneno aya
->Mimi ni mjinga sana
->Mimi ni mpuuzi na kilaza kiwango cha Sgr
->Mimi ni Zumbukoko nimepeleka mafao yangu kwenye kamari

->Mimi nina nyota ya umaskini

ukisha maliza kutamka ayo njoo nikupe odds 5 za uhakika ufute huo ujinga ulio jaa akilini mwako
Haha Haha.

Cc monopoly inc
 
Achana na mawazo ya kujiua sio solution ya matatizo yako, ukipitia changamoto yeyote acha kabisa kuwaza kifo kama suluhu, huo ni udhaifu uliotukuka.

Kama mimi nilipitia hayo na nikavuka licha ya maumivu makali kwanini wewe ushindwe?

Uza simu anza upya tafuta cha kufanya kadri muda unavyoenda mambo yatakuwa sawa.

Epuka kuazima hela kwa watu na kuahidi kurejesha ukiwa na hiyo simu yenye uwezo wa kukufanya ucheze aviator, kwa sasa hata ukipewa hela utakimbilia kucheza tena(najua hili wengi watakataa/utakataa) ila nimepitia na ninajua kwa kuyaona kwa wengi. Jijenge mwenyewe taratibu taratibu na usifosi uazime hela usiomudu kurudisha, utajivunjia uaminifu na upo kwenye kipindi kigumu cha kusimama upya kuna muda utahitaji msaada na wakukusaidia ndio hao wanaokuamini, usiwapoteze.

Nakuandikia magazeti kwa sababu nimeyapitia haya na sipendi kuona mtu anayapitia naelewa maumivu yake.
Duuh...brother unanielewa sana.

Hii simu kweli kuendelea kuwa nayo nikipata pesa nitacheza tu, bora nisiwe nayo kwa sasa.
 
Najua nakosea Ila ndivyo ninavyo waona watu wanao beti

Huwa nawaona Kama hawako timamu na wavivu
Kwa mtazamo wako huenda ukawa sahihi.

Maana nakumbuka fainali ya world cup mwaka 2022 kati ARGENTINA na UFARANSA.

Msanii drake wa marekani alibeti dau la dolar milion moja (Tsh 2.3 bilion) na kumpa argentina ashinde.

Lakini kilichofata mechi ilitoka draw kwenye 90 minutes hivyo akapoteza tsh 2.3 bilion.

Ila kwake haikuwa shida maana ni sawa na alichukua 1000 katika laki akabetia.
 
Ninachoshukuru sijui kuendesha kindege, sijui kuzungusha lile tairi na wala sijui kucheza dubwi la mchina.

Ila kuna siku nimewahi kupoteza laki 2 kizembe sana ilikuwa 2020 kama sikosei.

Ni kupitia 1xbet nilikuwa nimebet football nikala.
Sasa ukatokea ujumbe kuwa naweza kudouble my winning, nikakubali.
Ukaja mchezo wa kupiga penalt halafu kuna goalkeeper anadaka.

Ninachokumbuka nilikula kama mara 2 tu, nyingine goalkeeper alikuwa anadaka na kutema hadi nikakauka kau.
[emoji3][emoji3]
 
FB_IMG_1709182982732.jpg
FB_IMG_1709182967949.jpg
 
Back
Top Bottom