Sumbi Sanchez
Senior Member
- Apr 16, 2017
- 100
- 355
Kamari (Au ni Kamali?) sio kitu cha kushiriki. Mchezo wowote wa kamari umetengenezwa kwa umakini mno wa kuipa mapato kampuni ya kamari. The Odds are always against you.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23]Bora hata usikijue maana ukikijua unaweza kukijaribu.
Ukiingia kinakutamanisha kwa kukupa pesa kubwa ndani ya dakika moja alafu ukinogewa ujue ndiyo unafilisika.
Akilia inakuja kuzinduka una buku kutoka milion
Hapana mkuu..sichezag kamaliSema ueleweshwe mzee sio kulaumu tuu au unaliwa sana kamari ukibet
Kama umeona ni kitu cha kutunga ni sawa.Hujui kutunga story vizuri. Kaa chini utunge kwa utulivu na uandike kwa hisia tukuonee huruma.
😭😭😭Umemsliza kabisa. Kale kamchezo ukiona umekula pesa kubwa ukatoa usirudie kucheza ukirudi tu umeumia.
Huyu jamaa ajiandae kisaikolijia hayo yote uliyomuambia ni kweli kabisa hakuna rangi hataacha kuziona
Kwa mtu aliewahincheza huo mchezo hawezi kukubaluana na wewe.Hii nayo ni ID yako pia au wewe ni Chawa? Inahitaji akili ndogo tu ya darasa la 2 kujua hii ni Fiction.
Hayo mawazo ya kujiua yafute kabisa maana unayaruhusu we mwenyewe, anza upya tafuta kibarua cha kujimudu, jipange jipe muda then tafuta mwanamke wa kuanza nae maisha, kamari hiyo ya hivyo acha kabisa bora ubet mpira kuliko hayo ma aviator.Nishifikia asilimia 95 ya mawazo ya kujiua siku nilipomalizwa kabisa nikabaki na zero.
Ila kwa sasa niko 60 % karibu na kujiuq.
Hasa nikiwaza namna ya kuipata tena hiyo pesa, sina kazi, umri umesonga sijaoa ndiyo kunanipa stress kabisa.
We jua tu nilifukuzwa nikalipwa mafao shetani akanipenda akanipeleka kwenye kamari.Nini sababu ya kufukuzwa kazi? Isikute ulishaanza kuwehuka kitambo tu.
Nice words.Hayo mawazo ya kujiua yafute kabisa maana unayaruhusu we mwenyewe, anza upya tafuta kibarua cha kujimudu, jipange jipe muda then tafuta mwanamke wa kuanza nae maisha, kamari hiyo ya hivyo acha kabisa bora ubet mpira kuliko hayo ma aviator.
Naelewa situation yako maana hata mim nilipitia haya lakini nikavuka salama. Kukata tamaa ni mwiko kumbuka sababu ni tamaa zako, R I P kwa hela zote zilizopotea ukiwa unatafuta hela.
Aisee katika kitu namshukuru Mungu mimi ni mgumu sana kukata tamaa hata niwe kwenye gumu gani najua nitavuka tu hata kama litanigharimu na kuniumiza. We mkamaria kama umeweza maumivu ya kupoteza unashindwaje kuanza upya? Komaa kiume dunia na mafanikio haiitaji watu wanyonge, be strong meeeeeen, act tough meeeeeen.
Sawa mkuu,hivi ni dhambi eehHapana mkuu..sichezag kamali
Mbona zako waga unatunga na bado tunasoma, Kwahiyo unataka uendelee kutunga wewe tu au sioHii nayo ni ID yako pia au wewe ni Chawa? Inahitaji akili ndogo tu ya darasa la 2 kujua hii ni Fiction.
Achana na mawazo ya kujiua sio solution ya matatizo yako, ukipitia changamoto yeyote acha kabisa kuwaza kifo kama suluhu, huo ni udhaifu uliotukuka.Nice words.
Mpaka hapa nahisi nimepunguza asilimia kadhaa za karibu na kifo.
MI siandiki msome.Mbona zako waga unatunga na bado tunasoma, Kwahiyo unataka uendelee kutunga wewe tu au sio
Kama katunga fresh, sie hayatuhusu kikubwa alichotunga kuna watu kinawatokea kwenye real life kila siku
Muda muda muda muda.Nakuelewa kwa sababu unayopitia yanatokea kwa vijana wengi sana ila wengi wao hawasemi tu
Kupitia betting kuna watu hadi leo wamekuwa vichaa kutokana na kushindwa Ku handle madhara ya kisaikolojia waliyoyapata huko
wapo baadhi ambao tunawajua kabisa kuwa yule kawa chizi kutokana na betting/kamari baada ya kupoteza pesa nyingi au mali Fulani
Kwahiyo kwako hakuna kipya ni rejeo tu la kinachotokea kila siku na wengine wanasalimika baada ya kupata kadhia kama yako kwa sababu ndio huacha mazima Kamali
Betting/kamari ina uraibu mbaya sana bora ata vilevi vingine, hivo hii loss uliyopata tumia kama njia ya kujitathimini na fundisho kwa sababu pesa zinatafutwa tu na sio issue sana, issue ni kupoteza Muda
Epuka mawazo ya kusema IPO siku utakuja kurudisha hiyo 7.5M kupitia betting, hiyo hela sio nyingi sana wala wala sio ndogo sana na unaweza kuipata kupitia betting, ila unaweza kuja kupata 7M wewe ukiwa umeliwa 50M
Kwenye betting in long run, waga asilimia kubwa ni hasara tu kwa yule anaebett na Faida kwa kampuni anayotumia kubeti, itabakia kuwa addiction tu kuwa mtu hawezi kuacha kubeti ila ukweli kashapigwa sana za USO, ila akila anafarijika sana kumbe analishwa Chambo
ni concept pana kidogo kuwa hii kuwa dhambi au lah!!Sawa mkuu,hivi ni dhambi eeh
Miaka 20 iliyopita nikiwa na umri wako huo nilipata janga kubwa sana nikaona dunia si yangu tena. Nilifanya upambavu mkubwa sana na nikapoteza kazi nzuri huku jela ikinisubiri. Hapo nina familia na wananitegemea mimi, nilichukua uamuzi wa kujitoa roho, nikanunua frajili 20, nikachukua bia (Tusker) moja nikachanganya na Konyagi nikabugia yote. Nilikwenda kuponea hospitali kwa msaada mkubwa wa wife. Leo maisha yanaendelea na yote yaliyopita yalishapita. Tulia jipange upya, maisha ni zawadi muhimu sana na thamani yake haipimiki, tunapaswa kuyakumbatia kwa nguvu zetu zote hadi pale yatakapoondolewa kwetu.Nashindwa kuwaambia jinsi nilivyojikatia tamaa kiasi cha kuwa kichaa.
Ila ninachoweza kuwaambia tu vijana wenzangu tuacheni kubeti kwa malengo kwamba tunapata pesa huko haraka haraka.
Fikiria nimefanya kazi ya kuajiriwa kwa miaka 8, nikafukuzwa kazi nikaenda NSSF nikachukua milion 7.5 niliyokuwa nakatwa alafu yote nimeimaliza kwenye kindege cha aviator ndani ya siku 5 tu.
Nahisi kuna roho flani iliniongoza kwa sababu kwa akili ya kawaida najiona siyo mimi.
Lengo ilikuwa kubetia elfu 50 kama mtaji wa kubetia lakini kilichofata ni kupoteza milion 7.5 zote bila kubaki hata mia ndani ya siku 5 tu.
Hapa nilipo I wish hata nijitoe roho tu maana sijui ni wapi naanzia maisha tena pesa yote nishaipoteza kwenye uraibu wa kamari.
Kila nikiwaza nna miaka 30, sijaoa, sina biashara yoyote niliyoisimamisha kunilinda, sina maisha, kwa kifupi hiyo milion 7.5 nilitegemea ndiyo niingie nayo mtaani inilinde.
Lakini shetani kanikamata na kunikanda kisawa sawa.
Najiona mjinga wa kiwango cha Phd ndiyo maana nimejiita Zero Brainer, sina wa kumlaumu ila tujiepushe sana na uraibu hasa wa kubeti.
Mimi naweza nikafa leo ila sitaki vijana wenzangu yaje yawakute yaliyonikuta mimi sasahivi.
Mimi hali nnayopitia sasa kwa sababu ya kubeti nakosa maneno ya kuwaelezea ila siku nikifa mjua KINDEGE cha AVIATOR kimesababisha kifo changu .